Smiles
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 1,231
- 107
05 August 2010
Joyce Joliga, Songea
WAFUASI wa Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Dk Willibrod Slaa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakisubiri kumdhamini Rais Jakaya Kikwete nusura wazue mtafaruku walipopishana na kuzomeana.
Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 6:30 mchana wakati wafuasi wa Chadema walipokuwa wametoka kumpokea Dk Slaa uwanja wa ndege wakapishana katika eneo la ofisi za CCM mkoa walipokuwapo wale wa CCM wakisubiri kumdhamini Rais Kikwete katika harakati zake za urais.
Walikuwa wafuasi wa Chadema walioanza kuonyesha alama za vidole viwili juu huku wakiwazomea wenzao waliokuwapo ofisini hapo ndipo wale wa CCM nao wakawajibu zikazuka kelele kwa muda lakini baadaye wakawa wameachana.
Wanachama na wafuasi wa Chadema waliwazomea wenzao wakidai kuwa wametelekezwa na Rais Kikwete kwa kumdhamini picha wakati yeye mwenyewe hakuwapo na kwamba asingefika kwa hiyo waliuziwa mbuzi kwenye gunia.
Naye Dk Slaa aliwataka watumishi wa serikali mkoani Ruvuma kukipigia kura chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao baada ya Rais Kikwete kuzikataa hadharani kura za watumishi 350,000 mapema mwaka huu.
Alisema kauli hiyo ya Rais Kikwete imeonyesha kuwa nyuma ya wafanyakazi hao kuna ndugu, jamaa na wazazi wanaowategemea na ambao wanahitaji nyongeza hiyo ya mshahara kujikimu kimaisha.
Dk Slaa aliyasema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya Songea kwenye viwanja vya soko la Bombambili mjini Songea ambako maelfu ya wananchi walijitokeza kwa wingi kumpokea.
Dk Slaa alisema Chadema imejipanga kuwatetea wafanyakazi na kutatua kero mbali mbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kukomesha ufisadi kwa vitendo.
Alipokewa kwa maandamano ya watu na pikipiki zilizopambwa kwa bendera ya Chadema na magari ambayo yalivuta umati wa watu kuja kuiona helkopta yake na kumsikiliza.
Dk Slaa ambaye alifika mkoani Ruvuma kwa lengo la kutafuta wadhamini baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais, alisema wafanyakazi wasijisikie wakiwa bali wakipigie Chadema kura katika uchaguzi ujao ili kiwakomboe.
"Tunaomba mahakimu, askari ,walimu na hata wafanyakazi wa Ikulu mtupigie kura Chadema katika uchaguzi mkuu kwani sisi tunazithamini sana kura zenu na tuna imani iwapo mtatupigia kura pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zenu, tutaingia Ikulu kwa kishindo," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa aliongeza kuwa Chadema imejipanga kushughulikia matatizo ya wafanyakazi hivyo amewatoa wasiwasi wafanyakazi na kuahidi kushugulikia matatizo yao pamoja na yale ya wakulima na wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine Dk Slaa ameponda ziara za Rais Kikwete nje ya nchi akisema kuwa hazina tija kwa taifa na watanzania kwa ujumla.
Alisema tofauti na mawazo ya wengi, ziara hizo za Rais haziwanufaishi wananchi bali zinaendelea kuwaacha katika lindi la umaskini huku wageni kutoka nje, wakiendelea kunufaika na madini na utajiri mkubwa wa raslimali za nchi.
"Sihitaji kusema idadi ya safari ambazo Rais Kikwete amezifanya nje ya nchi kwani hata nyinyi mnazifahamu. Ninachoweza kusema tu ni kwamba ziara hizi hazijazaa chochote zaidi ya dhahabu zetu kuendelea kuchotwa na wageni wakati Rais akinywa chai nzito nje ya nchi,"
"Hivyo nawaomba mfanye mabadiliko na kukipigia kura Chadema ili tuweze kuwaletea maisha bora na kushugulikia kero na matatizo yenu,"alisema Dk Slaa
Awali mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime amewataka wananchi wa mkoa wa Ruvuma kufanya mabadiliko kuchagua chama hicho .
Dk Slaa aliondoka Ruvuma jana mchana na kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya kuendelea kufatuta wadhamini huku akiahidi kurudi tena Ruvuma wakati wa kampeni.
Katika hatua nyingine Dk Slaa aliponda Kilimo Kwanza kwa kwa kikielezea kuwa ni nyimbo tu kwani wakulima hawajashirikishwa ipasavyo kushiriki utekelezaji wake.
CHANZO: Mwananchi