Wafuatao, ndio watu pekee wanaoijua kesho yao!

Wangekuwa wanayajua ya Kesho mbona makampuni ya kubeti yangefilisika
WALOKOLE hawaishi MAISHA ya kubahatisha. ( Betting).

Kubeti ndio kamari yenyewe, na kamari ni abomination, wana wa Mungu wamezuiwa kubeti.

MAISHA ni halisi SI bahati nasibu.

Asiyefanya kazi na asile.
 

MK254 unakwitwa huku
 
elezea utakatifu ninini?
Kisha elezea utakatifu wako
Nimeelewa vyema rudia kusoma kilichoandikwa hapo juu 🙄

Kutubu DHAMBI na kuziacha, ukajazwa Roho mtakatifu baada ya kumwamini Yesu ndio utakatifu huo.

Roho mtakatifu huishi ndani ya waliomwamini Yesu, ndio awafanyaye wawe watakatifu.

Pata vazi la wokovu🙏
 
Chai

Nimeishia hapo kwenye mlokole ni IMMORTAL
Ni kweli,

Mlokole ni Immortal. Kama huamini, nenda chukua nyayo za mguu wa Mlokole, mpelekee mganga kama atasomeka kwenye rada zao.
 
Ni kweli,

Mlokole ni Immortal. Kama huamini, nenda chukua nyayo za mguu wa Mlokole, mpelekee mganga kama atasomeka kwenye rada zao.
Nipe majina yako pm nikakuoneshe kitu kama unajiamini
 
Nipe majina yako pm nikakuoneshe kitu kama unajiamini
Nimekwambia hivi,

Mlokole harogeki, kumroga Mlokole, uanze kumroga Yesu aliye ndani ya Mlokole, jambo Hilo shetani hawezi kujaribu.
 
Nimekwambia hivi,

Mlokole harogeki, kumroga Mlokole, uanze kumroga Yesu aliye ndani ya Mlokole, jambo Hilo shetani hawezi kujaribu.
umehamia kwenye kuroga tena, umesema mlokole ni IMMORTAL labda huelewi maana ya IMMORTAL ndugu, maana yake mlokole hawezi kufa! je, ni kweli mlokole hawezi kufa? mimi sijasema habari za kurogeka nazungumzia uIMMORTAL, hata BWANA alisema "Hakika mtakufa" wewe ni nani unapotosha watu kwamba walokole ni IMMORTAL.
 
Rudia kusoma kifungu nilichoquote John 5:24.

" Amekwisha pita toka mautini kwenda uzimani"

Labda tuanzie hapa,

Kufa ni Nini?
 
Walokole mna utaahira sana
 
Aaah em wacha hizo wewe mambo kwa ground sio kama usemavyo mkuu.
Ndio nakwambia,

Zinaa ni kitendo kinachofanyika kwenye mwili wa mtu,

Sasa mwili wa MLOKOLE ni hekalu la Mungu Roho mtakatifu, sasa haliwezekani hekalu Hilo liwe pia hekalu la shetani wa zinaa. Ukiona Mlokole azini, huyo ni fake, Roho mtakatifu hayumo ndani yake.
 
Walokole mna utaahira sana
Ni kweli,

Lazima uwepo tofauti kati ya wana wa Mungu na wana wa Ibilisi, watenda maovu, uzao wa nyoka.

Nakuombea uokoke, uwe na hakika juu ya kesho yako.

Ubarikiwe 🙏
 
Kesho ya mchawi ambaye ataamua kumkataa Yesu na kuendelea kuroga inafahamika,

Ni kuzimu, Kisha jehanum ikiwa atafia Dhambini.
 
Rudia kusoma kifungu nilichoquote John 5:24.

" Amekwisha pita toka mautini kwenda uzimani"

Labda tuanzie hapa,

Kufa ni Nini?
kurudi mavumbini kulala usingizi baada ya pumzi ya roho kuuacha mwili mtu anayarudia mavumbi anakuwa mavumbi anazikwa haendi popote analala kaburini kusubiri siku ya hukumu, ambapo kila mmoja alielala ataamka wengine kwa uamsho wa kuhukumiwa wengine kwa uamsho wa kukombolewa.
 
Pumzi ya uhai kwa hiyo inakufa pia Roho ijitengapo na mwili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…