Wafugaji kuku mtabadilika lini?


Hivi hiyo bei ya 5500 ni wapi nami nikimbie upesi nikanunue!!??
 
Soko ndio linaloamua bei sidhani kama kuna mfugaji anataka kuuza kwa bei ndogo....kama bei iliyopo sokoni ni sh 5000 wewe ukikomaa na kuuza 9000 nani atanunua!

Mimi nauza tshs 10000,na wananunua watu wengi sana.sema kila MTU ana mtandao wake kibiashara
 
Wakati walaji wanaongezeka wafugaji nao wanaongezeka.
 
Wakati walaji wanaongezeka wafugaji nao wanaongezeka.
 
Kinachosababisha bei ikae constant kwa mda mrefu ni ongezeko la usawa baina watumiaji na Idadi ya kuku kutoka kwa wafugaji. Huwezi kuuza bei zaidi ya soko linavyohitaji, hata hivyo kabla ya kuuza bidhaa kwa dalali ni vizuri ukafanya uchunguzi bidhaa yako inahitajika kwa kiasi gani sokoni. Tatizo la biashara kama hizi ni kwamba ni biashara rahisi kuifikiri ukiwa na kamtaji hali inayosababisha ongezeko la supply sokoni sasa hata kama Idadi ya watumiaji inaongezeka unakuta uwiano hautofautiani sana kwa hiyo bei inacheza pale pale. Mfano mzuri ni bei ya kuku wa kienyeji wakati wa sikukuu ipo juu sababu ya demand yake ukilinganisha na supply.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…