Wafugaji ni kundi muhimu sana katika Duniani hii, bila wao hatupati nyama,maziwa,ngozi na mboleya ya samadi.
Kwa Tanzania makabila ambayo ni maarufu kwa ufugaji ni Wasukuma,wamasai,wataturu nk
lengo langu siyo kuwachafua wafugaji ila nataka jamii ifahamu kuwa kuna baadhi ya wafugaji hawajali kabisa utu wa wanadamu wengine.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo niliyojionea mwenyewe yakitendeka katika jamii hizi za wafugaji.
Binti kupiga magoti kwa muda mrefu pindi ahudumiapo wanaume.
kwa nini binadamu mwenzako apige magoti kwa muda mrefu ili kukusubiri wewe umalize kunywa maji na wakati mwingine unakuta muhudumiwaji anakunywa maji huku anamazungumzo kadhaa na wenzake au unakuta wanaume wapo wengi hivyo binti atapiga goti muda mrefu mpaka wamalize kunywa ndipo achukue vyombo vyake na kuondoka navyo.
Na kuna wakati magoti anaanza kupiga mbali halafu ndiyo anakuja kwa kutembelea magoti ili kuwahudumia wanaume.
Huu ni ukatili na tena ni unyanyasaji unaohitaji kukemewa na watu wote. Mfano Pawaga Iringa,madibila nimeiona hii hali
Binti kuolewa kwa ng'ombe nyingi.
sina maana ya kupinga utoaji wa mahali ila mahali ikiwa kubwa sana inasababisha huyu binti aende kupata tabu huko aolewako kwa sababu itabidi akazae sana na afanye kazi sana ili kifidia idadi ya ng'ombe walizochukua wazazi wake.
Mfano unakuta binti ameolewa kwa ng'ombe 37,30,40 au zaidi hii siyo mahali Bali ni biashara.
Madhara yake ikitokea huyu binti anapitia changamoto katika ndoa yake hawezi kurudi nyumbani na hata akirudi hawezi pokelewa na wazazi wake kwa sababu tu eti hawana ng'ombe za kurudisha na hivyo avumilie tu kwa manyanyaso ya aina yoyote.
Binti akiolewa haruhusiwi kwenda kuwasalimia wazazi wake mpaka ipite miaka 5 na kuendelea.
Kama hakuna msiba wa baba au mama huyu binti anaweza kukaa hata miaka 10 bila kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Ataruhusiwa pindi tu atakapokuwa ameshazaa watoto kadhaa.
Mfano hili nimeliona kwa wasukuma walioko bonde la usangu mbarari.
Kuwepo kwa chagulaga,
chagulaga ni utamaduni unaopatikana huku usukumani ambapo vijana wengi waliobeba fimbo wanamkimbiza binti pindi atokapo aidha kusaga mashineni,mnadani,ngomani au harusini. Kwa hiyo wakimuona wanaanza kumkimbiza na wakimpata wanamzunguka na Kisha wanamwambia "chagulaga mayu" yaani chagua mama yule binti akimgusa kijana mmoja basi wengine wanasimama pembeni ili kumpa nafasi mwenzao aelewane na yule binti.
Yule binti wakisha zungumza na kupanga anaanza kuondoka na jamaa wanamfuata tena na kumtaka amchague mwingine tena kwa hiyo unakuta binti anafika kwao kwa kuchelewa lakini akiwa amechoka wakati mwingine anachafuka kwa kudondoka sababu ya kukimbia.
Utamaduni huu ni kero na unakera sana kwa sababu unamfanya binti anakuwa kama mpira wa Kona kila mwanaume anamgombania
Mfano njoo Utengule hata sasa utayaona haya
Wananyimwa haki ya kupata elimu.
Elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto lakini katika jamii za wafugaji zimekuwa hazitaki na hazioni umuhimu wa kuwapeleka watoto shule. Mtoto hatakama kafaulu sekondari wazazi wake wako tayari kutoa chochote ili mradi mtoto asiende shule na lengo lao ni kutaka mtoto abaki nyumbani ili aolewe.
Mfano Wataturu walioko Igunga hapa Makomelo na maeneo mengine
Mtoto wa kiume ananguvu kubwa kimamlaka kuliko mtoto wa kike hata kama huyo wa kike ni mkubwa
Mtoto wa kike anatakiwa atii,asikilize na afuate maagizo yoyote yanayotolewa na mtoto wa kiume hata kama wa kiume ni mdogo kiumri.
Mtoto wa kike hasikilizwi na haaminiwi katika jamii hizi za kifugaji, ndiyo maana mtoto wa kiume anapewa sauti ya maamuzi mapema sana na anaweza kumwadhibu dada yake muda wowote hata kama dada ni mkubwa kuliko yeye.
Mfano nimeona nilipokuwa Bukundi mkoani Simiyu kijana anamchapa dada yake ambaye hata hawakaribiani kiumri lakini anamwazibu huku wazazi wakitizama tu na kisa chenyewe eti dada hajawatengea mboga nzuri wageni wa yule kijana.
Mwisho, Hizi jamii za kifugaji ziangaliwe kwa jicho la kitofauti ili ziweze kuwapatia haki zao mabinti badala ya kuwakandamiza na kuwaona kama wao ni kitega uchumi.
Nasema hivi kwa sababu nimeona binti akiozwa licha ya kuwa na ufauru mzuri wa kwenda kidato cha tano na alikuwa amefaulu kwa divition two lakini aliolewa na ndoto yake ya kusoma ikaishia hapo.

Upvote
1