Jamani nimekaa nikajiuliza inapotokea mtu akafungwa Jela, na alikuwa na mke/mume je hatma ya ndoa yao ikoje? Je anayebaki uraiani anatakiwa asipate unyumba hadi kifungo cha mwenzi wake kiishe mfano Miaka 15? Je kiubinadamu inawezekana kuvumilia kwa muda wote huo hata kama unajilinda? Haki ya wanaobaki uraiani ikoje? Na km akitoka nje kuna ubaya au afanyaje?
Hata magereza ya bongo kulikuwa na vyumba maalumu vya wafungwa kukutana na wenza wao ila kwa sasa vimebomolewa na serekali imeongeza vyumba ya kulala wafungwa
Kuna haja ya kuangalia haki za wafungwa ikiwa ni pamoja na kuwapa haki ya kukutana na wenzi wao wa ndoa. Kifungo hakijamuondolea haki hiyo.Kama tuna nia basi hili linawezekana. tatizo letu ni ukosefu wa ubunifu katika mfumo wa magereza yetu na ni moja ya majukumu ya tume ya haki za binadamu.