Mheshimiwa Nanyaro anasema kuwa rufaa ya Mramba na Yona haikumalizika siku ile ya tarehe 28/11/08 hivyo ilibidi waletwe Mahakama Kuu kumalizia rufaa yao siku ya Jumatatu tarehe 1/12/08. Akaongezea kuwa kwa kuwa akina Mramba walimaliza shughuli zao pale Mahakama kuu basi ilibidi wapelekwe pale Kisutu watafutiwe mahali salama wakae wakisubiri watuhumiwa wengine wamalize kesi zao pale Kisutu ndo warudishwe Keko na hawakwenda kisutu kwa ajili ya dhamana. Hii ni kwa mujibu wa bwana Nanyaro. lakini kwa ufahamu wangu mimi, mtuhumiwa amalizapo shughuli zake na Hakimu/Jaji, na akatakiwa kurudi mahabusu, basi hurudishwa mahabusu ndogo pale mahakamani kusubiri gari (karandinga, siku hizi kuna marco polo) la kuwarudisha keko, ukonga segerea etc Hayo yote alitaka kujitetea tu. Issue atuambie watu walipataje simu huko gerezani na niwafungwa sio mahabusu. Ama wanawapeleka mjini kufanya shopping halafu wanawarudisha tena huko gerezani?