Wafungwa wapatao 130 watoroka jela nchini Ethiopia

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Takriban nusu ya wale waliotoroka kutoka jela nchini Ethiopia mapema asubuhi ya Jumatano bado hawajapatikana.

Kwa jumla, wafungwa 130 walitoroka jela katika mji wa Nefas Mewcha katika eneo la Amhara.

Walisaidiwa na wale wanaodai kuwa wanachama wa wanamgambo wa Fano ambao wamekuwa wakipigana pamoja na serikali katika vita dhidi ya waasi katika eneo jirani la Tigray.

Kamishna wa polisi wa eneo hilo, Tekola Ayifokeru, aliambia BBC watu hao waliokuwa na silaha, ambao walisafiri kwa magari matatu, pia walivamia ghala la kuhifadhia silaha na kupora. Alisema wafungwa 65 wamekamatwa, washambuliaji 16 wameuawa na polisi watatu wamejeruhiwa.

Kamanda huyo alisema kuwa jaribio kama hilo lilifanywa wiki iliyopita kwenye gereza la takriban kilomita 325 (maili 200) kusini-magharibi mwa Nefas Mewcha katika jiji la Finote Selam.
 
Hawa watu mara nyingi huwa wanapenda sana kukimbilia Tanzania. Tuwe waangalifu sasa wasije wakaingia nchini mwetu; mtu mhalifu ametoroka kwao halafu akiingia nchini mwetu kama mhamiaji haramu inakuwa ni hatari zaidi kwetu sisi
 
Back
Top Bottom