Nyati
JF-Expert Member
- Mar 6, 2009
- 2,521
- 1,906
Wakuu Salaam,
Jana usiku niliangalia kipindi cha Star TV ambapo mmoja wa waganga wa kienyeji alikuwa ananadi dawa zake pamoja na huduma nyingine anazozitoa. Kwa ujumla ni kama vile jamii yetu imechanganyikiwa na kila mtu anatumia kila njia kuhamisha umiliki wa fedha kutoka kila mahali hadi mfukoni mwake.
Jamaa anasema ukienda kwake yeye anaangalia kucha tu na kukutabilia maisha yako ya baadaye, anasema hata ukimpeleka mwanao yeye atakutabiria na kukupa ushauri na madawa ili afanikiwe maishani mwake kupitia kusoma KUCHA zake. Baadaye pia aliongelea kusoma macho na kutoa tabiri hizo hizo!!!
Alikuwa hana ajenda maalumu bali kurukia vitu mbali mbali kufanikiwa maishani, magonjwa ya macho, uzazi, nguvu za kiume, viagra, kupata watoto, n.k. Alikuwa anajitahidi kuongea kiingereza kwa shida
Kwa kweli nimesikitishwa na hali hii ambayo sasa imeshika kasi lakini nashangaa inakuwaje wamiliki wanatoa muda (hata kama ni kwa pesa ) kwa watu kama hawa???!!!!!!.
Huhitaji kupiga ramli kujua kuwa ni wapotoshaji wakubwa hawa. Kama kuna mwana JF ambaye anafanya kazi ktika vituo hivi, naomba atujuze hasa ni kwa nini wanaruhusiwa, Je uwa mnahakiki wanachoongea ama mnajali pesa tu.
Nawasilisha