Elections 2010 Waganga wa kienyeji wa wagombea; huwezi kuamini

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Ati mgombea mmoja wa urais waganga wake wamedhibitiwa na mmoja wa watu wake wa karibu kiasi kwamba ameambiwa hawezi kumtimua huyo jamaa kwa sababu akimtimua tu mambo yake yataenda kombo. Kumbe yule jamaa imedokezwa kuwa amewalipa waganga hao kiasi kikubwa cha fedha ili wamuambie mgombea huyo habari hizo kuwa "fulani ndiyo nyota yako, ukimuondoa tu na wewe umekwisha".

Ukiondoa huo baadhi ya wagombea wengine wameanza kutembelea "washauri hawa" kwani Sheria ya Gharama za Uchaguzi haikatazi gharama za ushauri!!!!
 
Kumbe kweli Siasa mchezo mchafu..nadhani kwa asilimia kubwa Taifa hili tunaongozwa kwa nguvu za giza ndio maana mambo yanaharibika...................
 
Ati mgombea mmoja wa urais waganga wake wamedhibitiwa na mmoja wa watu wake wa karibu kiasi kwamba ameambiwa hawezi kumtimua huyo jamaa kwa sababu akimtimua tu mambo yake yataenda kombo. Kumbe yule jamaa imedokezwa kuwa amewalipa waganga hao kiasi kikubwa cha fedha ili wamuambie mgombea huyo habari hizo kuwa "fulani ndiyo nyota yako, ukimuondoa tu na wewe umekwisha".

Ukiondoa huo baadhi ya wagombea wengine wameanza kutembelea "washauri hawa" kwani Sheria ya Gharama za Uchaguzi haikatazi gharama za ushauri!!!!

mambo ya kutisha haya
 
Huyo mgombea atakuwa anatoka katika chama jeuri 'CHADEMA'
 
Na hii yote ni ya wale wenyepesa na hawakubariki ndio kazi zao

sasa kama Kimbisa hakubariki Kondoa kwao kwanza, Jijini Dar hakubariki, Dodoma Mjini nako hakubariki analazimishia na kuwavuruga wanachama sasa wategemea ataacha kwenda kwa waganga wa kienyeji na kuhonga juu.

Jamini hizi siasa inaitaji ukalimu sana jamani kuongoza wananchi sio mchezo ati wao wanataka madaraka kwa nguvu zote
 
Ati mgombea mmoja wa urais waganga wake wamedhibitiwa na mmoja wa watu wake wa karibu kiasi kwamba ameambiwa hawezi kumtimua huyo jamaa kwa sababu akimtimua tu mambo yake yataenda kombo. Kumbe yule jamaa imedokezwa kuwa amewalipa waganga hao kiasi kikubwa cha fedha ili wamuambie mgombea huyo habari hizo kuwa "fulani ndiyo nyota yako, ukimuondoa tu na wewe umekwisha".

Ukiondoa huo baadhi ya wagombea wengine wameanza kutembelea "washauri hawa" kwani Sheria ya Gharama za Uchaguzi haikatazi gharama za ushauri!!!!
Mzee Mwanakijiji, habari hii haijakaa Ki Mwanakijiji, hii imekaa kwa stail ya magazeti pendwa (Udaku), ungeikikijisha japo kidogo, ifanane na Mwanakijiji Stlye unless kama ni Friday evening, but not for Monday morning.
Thanks anyway.
 
Mwanakijiji ..... Huwezi kuamini peke yako mie naamini zaidi ya hayo wanayoweza kufanyiwa waganga!

Waganga wanajenga majumba ya faghari ukimaliza uchaguzi

Hakuna uchaguzi bila uganga Tanzania ..... Umeshatinga bungeni zama nyingi sana
 
Kama wiki mbili zimepita nilikuwa nimeenda beach eneo la msasani club kujipumzisha nilikuwa nimechagua eneo ambalo halina mtu ili nipate utulivu ninao taka, akaja mzee mmoja na mfuko wake wa rambo alikuwa anataka kuoga na hivyo aliomba kuniachia mfuko wake nimwangalizie akiwa anaendelea kuoga, mimi nilianza kumchokoza yule mzee na maswali ya kwa nini anaoga baharini haogopi atazama, na je ni kawaida yake kuja kuoga msasani. Mzee yule aliniambia kwamba ndio kwanza amefika kutoka sumbawanga kwa ajili ya kazi ya waheshimiwa na ni lazima aje aoge baharini ili kufanya mambo yake sawa. nikamuuliza waheshimiwa gani hao, mzee hakuniambia kitu ila alinitolea kwenye rambo yake lundo la busness kadi za waheshimiwa wengi nilibaki mdomo wazi.

Nchi yetu inaendeshwa kishirikina kwa kweli.
 
Na hii yote ni ya wale wenyepesa na hawakubariki ndio kazi zao

sasa kama Kimbisa hakubariki Kondoa kwao kwanza, Jijini Dar hakubariki, Dodoma Mjini nako hakubariki analazimishia na kuwavuruga wanachama sasa wategemea ataacha kwenda kwa waganga wa kienyeji na kuhonga juu.

Jamini hizi siasa inaitaji ukalimu sana jamani kuongoza wananchi sio mchezo ati wao wanataka madaraka kwa nguvu zote

Mkuu, kwa kutumia neno 'hakubariki' ulikuwa una maanisha kwamba hajatoa baraka katika hizo sehemu (yaani, hajabariki) au? Au ulinuwia kuweka 'l' badala ya 'r' kumaanisha kuwa hakubaliki? Kwa sababu hiyo herufi moja inabadili kabisa maana ya post yako
 
Waganga wakienyeji ndio wanatembelea magari ya kifahari kama VX,RangeRover.Wateja wakawaida awawezi kumuwezesha mganga kununua VX bali mafisadi(Wanasiasa) ndio wanaweza kumpa pesa nyingi.:smash:
 
ndio maana hata kumaliza tatizo la albino haiwezekani, kwasababu walioko madarakani na kwenye vitengo ndio walioshikwa masikio na waganga wa kienyeji. Mungu na awaumbue kwa Jina la Yesu!
 
Mi naamini tuzidi kumuomba Mungu wetu pamoja na hayo mambo ya ulimwengu wa roho, kwani naamini siku moja zitz 'expire" na mambo yatakuwa hadharani!! :drum:
 
Back
Top Bottom