ANAUPIGA MWINGI
JF-Expert Member
- Apr 14, 2022
- 389
- 757
Sisi Watanzania tumekuwa tunaidharau sana nchi yetu na wengi tunapenda mara kwenda kuishi Ulaya au hata South Africa. Lakini Jambo ambalo hatujajua katika nchi zote 50+ za Africa, foregners wengi wanapendelea sana kuishi Tanzania na si kwingineko.
Zamani walipendelea sana kuishi Nairobi Kenya ila sasa hali imebadilika ni Tanzania wanapenda sana kuishi.
Wazungu kwa Waafrika kwa wa Asia wanapenda mno kuishi Tanzania. Ile Mahakama ya Mauji ya Rwanda ilipofungwa kule Arusha ndo nilijua hili, Wale Staff wengi kuna waliokuwa wanalia live kabisa kuondoka Tanzania na cha ajabu walikuwa washapita nchi nyingi ila kwa Tanzania walikuwa wanalia kabisa.
Pia Wageni wengi wanaofanya kazi kwa mikataba Tanzania huwa mikataba yao ikiisha acha kabisa kabisa utawahurumia si kwa kulia kule, kuna dada mmoja wa Denmark sitasahu alivyolia kisa kuondoka Tanzania yaani nilitamani nimuoe sema ndo kama hivyo.
Watalii wanaokuja Tanzania baadhi hurudi kuja kuishi kabisa na kuanzisha biashara hasa za Utalii. Arusha kampuni nyingi za utalii wale wanaomiliki kwanza walikuja kama Watalii na baadae wakarudi kuja kuishi.
Kuna Shirika moja nilifanya nalo kazi ni NGO ya kimataifa na ina-Oparate nchi nyingi sana za Afrika, sasa ilikuwa na Expert Wazungu na walikuwa wana-oparate project kwenye nchi zaidi ya 10 Afrika kama vile Kenya, Ghana, Cameroon, Rwanda, Malawi, Uganda, Zambia, Ethiopia na kadhalika. Ila walikuwa wanapenda kuishi Dar Es Salaam yaani ndo walipendelelea kuishi. Sasa zile project zilivyokuwa zina-face out walikuwa wanakomaa na proposal wapate pesa waendelee kuishi Tanzania.
Foregners kwetu ni fursa na wala si kwamba wanakuja kutuzibia riziki, bali tunatakiwa kuwatumia sana kwenye biashara kama za Real Estate, Biashara za vyakula na biashara za burudani.
Kwa Jiji kama Arusha, Dar na Zanzibar kuna Foregners wengi sana na Arusha ikiwa na wengi zaidi nadhani kuliko mji mwingine wowote ule Tanzania, hawa wanakula sana, Wanalala, wanakunywa hivyo ni fursa kwetu sisi. Watanzania tunachopaswa kufanya ni kuwageuza kuwa fursa na sio kubakia kuwatazama tu.
Kinachoumiza ni kwamba vitu wanavyokula sana vinatoka nje kama Kenya, Afrika Kusini na huko Egypt, ni aibu unakuta uyoga unatoka South Africa na Kenya, nyanya zinatoka South Africa.
Leo hii unakuta mfano Super Market kubwa kubwa Dar na Arusha may be ambako hawa Foregners ndo sehemu zao za manunuzi unakuta Super Market imejaa product za South Africa, Kenya na Misiri, hii sio sawa kabisa Watanzania yaani mfano Kenya wananufaika sana na hawa foregners kuliko sisi Wazawa, na hii tunaona ni sawa?
Hebu tuamke Watanzania kwa sababu hawa Foregners wanazidi kuongezeka kila kukicha, hawa tuwatumie tusibakie kuwashangaa mitaani, la sivyo watatumiwa na jirani zetu.
Tuzalishe vyakula standard vya kulisha hawa watu, kwenye Real Estate hakuna shida ila kwenye vyakula na bidhaa zingine tunakwama sana sisi Watanzania, hawa watu wanaongezeka sana yaani kuna Jam ya Foregners wanaokuja kukaaa Tanzania.
Hawa wanapenda kufuga hasa Mbwa na Paka, tuwazalishie sana mbwa na Paka. Wanapenda Garden tuwekeze kwenye Garden kwa wale wanaoweza. Wanapenda sana vyakula Organic tuzalishe Organic food tuwauzie.
Tujadili tunakwama wapi kuwatumia kama fursa? Nini shida? Nini kinahitajika?

Upvote
2