Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
Ukifunua vitabu vya sekondari kila definition utaona inaanza "it's greek Word" hata lugha rasmi ya Binomial nomenclature ni Greek tuseme Biology na sayansi kwa ujumla lugha yake ni Kigiriki.

Kwanini?
Asiilimia 70% ya wanafalsafa, Wanasayansi, Wagunduzi wote wanatoka Ugiriki. Kwa ufupi Sayansi imeanzia Misri ya kale na kutapakaa ulaya hasa ugiriki huko ndiko ilikofanyiwa kazi vizuri wewe chunguza kila mwanafalsafa anatoka Ugiriki.

Ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo mia moja ambapo kila mji ulikua na utawala wake, Mji wa Athens na Sparta ndio ilikua miji mikubwa na yenye nguvu zaidi, japo miji hii mra nyingi ilikua inapigana kwa ajili ya kugombania ardhi lakini vilikua vimejiunga pamoja ili kujilinda na uvamizi wa kutoka nje.

Enzi hizo Ugiriki ilikua Ugiriki kweli kuna madume ya haja hasa (Alpha, Beta peoples) mwaka 480 BC Mfalme Leonidas wa Sparta aliongoza jeshi la wanaume 300 tu kupambana na mfalme Xerxes kutoka Persia mwenye jeshi la watu 10000+ lakini waliwachinja hasa richa ya uchache wao. Japo Leonidas aliahindwa ila alijitahidi kuziwia uvamiI huo ambapo baadae Mfalme Xerxes alikuja kuuwawa na mrithi wa leonidas Themistocles

✓✓Kumbuka mfalme Xerxes ndio mfalme aliyemuoa Ester wa kwenye biblia ambae ester alitumia penzi kuziwia kuuwawa kwa Wayahudi wotewaliokua Babeli. (Kaa kumbukumbu zangu zipo sawa) Wafalme wa Persia waliitwa Ahasuerus. (Ahusuhero).

Sasa waku nini kiliwapata hawa watu? Gunduzi zote zilizofanywa kwao haziwanufaishi. Nilitegemea Ugiriki iwe miongoni mwa Super power county ila hata G7 haipo sijui G20.

Nini kiliwatokea? Sasa hivi hamna tena watu wenye akili au??
Esta 1:1-3
[1]Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba;
[2]siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Shushani ngomeni;
[3]mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; wakuu wa Uajemi na Umedi, watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake.
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.

1. Imhotep
2. Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
 
Hivi unajua sehemu kama Egypt, Mesopotamia, Crete, Syria, Anatolia, Iran, and the Indus Valley walipata civilization kabla hata ya wagiriki.

Pia wachina waligundua mengi na kusafiri hata kabla ya wengi ambao ndio wamekuwa accredited na ugunduzi huo.

Kwa ufupi ni utamaduni, kukiwa na utamaduni wa kuhoji na watu kupenda kujifunza basi jamii itagundua vitu na kuendelea (Binadamu wanazaliwa wakiwa a Blank Slate) Tabula Rasa ila jamii inayowazunguka ndio inawajengea wawe watu wa aina gani.

Iran ilikuwa imepiga hatua sana, lakini kuingia mambo ya imani all was destroyed in few years. Wachina walikuwa wamesafiri duniani kote tangia zamani ila Mfalme wao kupiga marufuku culture za nje ikawapunguzia kasi.

Kwahio na sisi hizi indoctrination kwamba kila kitu tumepewa au kila kitu kina sababu, hakuna kuhoji wala kutafuta ukweli usishangae miaka milioni moja ijayo tukawa bado tunapiga ramli na kudhani ni Jirani yetu katuloga, au tukiugua ni Mungu amependa.
 
Wagiriki walivyokua bado hawajaungana kila Eneo linajitawala walitumia nguvu zaidi kujiimarisha maana wao hawakugopa kufa waliaamini wao ni viumbe special kutoka kwa baba yao wa uumbaji Zeus. Majina mengi ya kigiriki yanaishia na S hata majina ya watu wa mataifai mengine yanaishia S kwakua ni utamaduni uliotokana na wagiriki. Yesu pia jina lake laishia na S yaani Jesus sababu ni kwamba wagiriki wanaamini majina yanayoishia na S yanamaanisha ni mwanaume kutokana na Mungu wao wa kiume Zeus jina lake lainshia na S

Walivyoungana na kua kitu kimoja wakaanza kutumia akili na nguvu ili kujiimarisha zaido kwa kila nyanja wafalme waliwatumia watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri katika kutatua changamoto zinazowakabiri na waliwekea mazingira wezeshi hapa sasa ndio gunduzi zikaanza.
Mfano......

Kipindi fulani ugiriki ilikua ni sherehe ya mavuno hivyo wagiriki walikua wanamsherehekea Mungu wao wa mavuno kuwapatia mavuno mengi. Mfalme kama kiongozi mkuu alitakiwa awepo kwenye sherehe sasa mfalme akampatia dhahabu Muhunzi (Goldsmith) amtengenezee kofia ya kuvaa wakati wa sherehe (Crown), Muhunzi kuona dhahabu kashikwa na tamaa akachakachua dhahabu akaweka dhahabu nusu akaongezea na bronze (shaba) akampelekea mfalme kofia yake.... Mfalme akaangalia kofia akaona hapa kashapigwa cha juu ila hana uhakika.

Akaamua kumuita jamaa mmoja ambae kipindi hicho aliaminika ana akili sana aje amchunguzie kofia yake kama imetengenezwa kwa dhahabu tupu kweli au imechanganywa. Ila akamwambia asiiharibu wakati wa kuichunguza maana hana kofia nyingine...Jamaa huyo ni Archimedes

Archimedes akachukua kofia akaenda maabala kwakwe akachunguza wee akashindwa kupata majibu kichwa kikawaka moto hajui afanye nini.. akamuagiza mfanyakazi wake amuwekee mai ya kuoga bafuni kwenye Jacuzzi.
Akaenda bafuni akavua nguo akaingia kwenye Jacuzzi maji yakamwagika nje aivyoona hivo akatoka nje akikimbia uchi huku anapiga kelele hadi ikulu.

Alipomfikia mfalme akaanza kusema harakaharaa "When a body is totally or partially immersed in a fluid is subjected to an upwards force equal to the weight of the displaced fluid. "

Mfalme akamwambia unamaanisha nini wewe mbona sikuelewi 😂😂
Ndio mzee baba akaanza kumuelezea vizuri sasa... Akachukua vipimo vyake akapima uzito wa dhahabu na Shaba kisha akapima uzito wa Ile kofia ikaonekana muhunzi aliiba dhahabu. Na hapo ndio tukapata Law pedwa ya Archimedes principle na law of floatation inayohusu Density. Kupitia law hizo tumepata Meli mbalimbali..

Sio hivyo tu Archimedes alisaidia san kwenye vita..alikua anatengeneza vifaa vya kivita au anatumia vioo kuunguza meli za maadui wanakuja kuvamia nchi yake.

Sisi huku kama una ujuzi wa kutengeneza Gobole au siraha unanyanganywa na unakomeshwa kabisa uwe mfano wengine wasirudie upuuzi kama huo
Hivi unajua sehemu kama Egypt, Mesopotamia, Crete, Syria, Anatolia, Iran, and the Indus Valley walipata civilization kabla hata ya wagiriki....

Pia wachina waligundua mengi na kusafiri hata kabla ya wengi ambao ndio wamekuwa accredited na ugunduzi huo...

Kwa ufupi ni utamaduni, kukiwa na utamaduni wa kuhoji na watu kupenda kujifunza basi jamii itagundua vitu na kuendelea (Binadamu wanazaliwa wakiwa a Blank Slate) Tabula Rasa ila jamii inayowazunguka ndio inawajengea wawe watu wa aina gani...

Iran ilikuwa imepiga hatua sana, lakini kuingia mambo ya imani all was destroyed in few years. Wachina walikuwa wamesafiri duniani kote tangia zamani ila Mfalme wao kupiga marufuku culture za nje ikawapunguzia kasi...

Kwahio na sisi hizi indoctrination kwamba kila kitu tumepewa au kila kitu kina sababu, hakuna kuhoji wala kutafuta ukweli usishangae miaka milioni moja ijayo tukawa bado tunapiga ramli na kudhani ni Jirani yetu katuloga, au tukiugua ni Mungu amependa.
 
Baada ya kuona Wana akili nyingi wakaamza kuweka sheria ngumu mpaka katika matumizi ya lugha. Kitendo cha kuweka sheria ya matumizi ya lugha ndicho kiliwagharimu mpaka leo
Sio kwamba Rumi ndio iliangushwa na lugha?? Ila Rumi wajanja waliachana na kutumia ubabe wakatawala watu kwa kutumia dini! Na wote tuseme amina 😆

Constantino mjanja sana nadhani aliona tawala ya Rumi inaenda kufa akaamua kutumia njia nyingine kutawala dunia. Si unaona watawala wa superpower county lazima wakapige chata kwanza Vatican 😆
 
Ukifunua vitabu vya sekondari kila definition utaona inaanza "it's greek Word" hata lugha rasmi ya Binomial nomenclature ni Greek tuseme Biology na sayansi kwa ujumla lugha yake ni Kigiriki.

Kwanini?
Asiilimia 70% ya wanafalsafa, Wanasayansi, Wagunduzi wote wanatoka Ugiriki. Kwa ufupi Sayansi imeanzia Misri ya kale na kutapakaa ulaya hasa ugiriki huko ndiko ilikofanyiwa kazi vizuri wewe chunguza kila mwanafalsafa anatoka Ugiriki.

Ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo mia moja ambapo kila mji ulikua na utawala wake, Mji wa Athens na Sparta ndio ilikua miji mikubwa na yenye nguvu zaidi, japo miji hii mra nyingi ilikua inapigana kwa ajili ya kugombania ardhi lakini vilikua vimejiunga pamoja ili kujilinda na uvamizi wa kutoka nje.

Enzi hizo Ugiriki ilikua Ugiriki kweli kuna madume ya haja hasa (Alpha, Beta peoples) mwaka 480 BC Mfalme Leonidas wa Sparta aliongoza jeshi la wanaume 300 tu kupambana na mfalme Xerxes kutoka Persia mwenye jeshi la watu 10000+ lakini waliwachinja hasa richa ya uchache wao. Japo Leonidas aliahindwa ila alijitahidi kuziwia uvamiI huo ambapo baadae Mfalme Xerxes alikuja kuuwawa na mrithi wa leonidas Themistocles

✓✓Kumbuka mfalme Xerxes ndio mfalme aliyemuoa Ester wa kwenye biblia ambae ester alitumia penzi kuziwia kuuwawa kwa Wayahudi wotewaliokua Babeli. (Kaa kumbukumbu zangu zipo sawa) Wafalme wa Persia waliitwa Ahasuerus. (Ashuru).

Sasa waku nini kiliwapata hawa watu? Gunduzi zote zilizofanywa kwao haziwanufaishi. Nilitegemea Ugiriki iwe miongoni mwa Super power county ila hata G7 haipo sijui G20.

Nini kiliwatokea? Sasa hivi hamna tena watu wenye akili au??
Nini kiliwakuta waTanzania? Hamna wapambanaji Kama akina kinjikitile,milambo,mkwawa na abushiri? Usiwazungumzie wenzako
 
Waarabu waligundua namba, na muda. Katika tiba Waarabu wameleta mabadiliko makubwa katika matumizi ya opium kumfanya mtu alale na tiba iendelee.
Sio Misri?? Maana katika namba kuna Wamaya,Wagiriki na wamisri.
Ila Alphabet ni Wamisri ndio walianzisha. Kwa warabu namfahamu Avicenna (Ibn Sina) kama polymath na baba wa tiba enzi zake
 
Waarabu walianzisha hesabu za aljebra
Kweli hapo nimechapia ase ila Gemetry imeanzia Misri ila mzee baba Pythagoras na Archimedes walizikuza zaidi.
Da Vinci alizitumia kuchora na kuficha details kweye mchoro wake wa Vitruvius Man.
Hichi kitu hapa chini hakin faida kwa Mwanadamu basi tu kukaririshana😆

220px-Quadratic_formula.svg.png
 
Ashuru ilikuwa dola nyingine kabisa wala haihusiani na dola ya Persia au Waajemi kama tuwaitavyo. Dola ya Waashuru iliitangulia dola ya Babeli as a superpower nation.

Wafalme wa Ashuru (Assyria) ni kama Sennacherib na Sargon. Dola ya Ashuru ilipoanguka ndipo Babeli ika rise as superpower commanding the then world.

Ikafata Dola ya Wamedi na Waajemi ambao hawa waliangusha utawala wa Babeli..hii dola nayo ikadumu hadi Alipokuja Alekzanda mkuu akiwa na dola ya kigiriki, kijana wa Philip wa Macedonia...akaiangusha dola ya Wamedi na Waajemi.

Wagiriki wakatawala ulimwengu ktk zama zao...Alexander alifika hadi Misri pale akajenga ule mji uitwao Alexandria uliopo mpaka leo...na alipoondoka hapo hakurudi tena. Alexander alifika hadi Modern day India akiwa na majeshi yake..wakishinda na kumiliki miji.

Alipotaka kwenda Hadi uchina..wanajeshi wakaasi..ikabidi waanze safari ya kurudi...alikufa akiwa kijana kabisa aged 32. Under him the Greek culture flourished, Alexander mwenyewe alifundishwa elimu na Aristotle mwenyewe.

Katika conquest zote, bwn. Alexander alitumia farasi wake mmoja tu aliyempenda sana aliitwa Bucephalus, alipokufa huyu farasi, Alexander akauita mji jina la farasi huyu huko India kwa kumbukumbu ya farasi wake.

Alipokufa bwn. Alexander utawala wake ukaganyika into four sections chini ya majemedari wake...ukaenda hivyo uki decline hadi Warumi walipoibuka 168BC as superpower.

Warumi nao wakatawala dunia kwa mkono wa chuma...hadi 476 dola yao ilipoanguka. Dola ya Warumi ilipoanguka ndipo zikatokea modern European states zilizodumu hadi Leo. Hizi zitadumu hadi mwisho wa historia ya dunia. Na baada ya hapo kwa mujibu wa unabii wa kitabu cha Daniel, unangojewa ufalme usio na mwisho, wa Bwana wa Mabwana, Mungu wa miungu...Yesu Kristo.

Point ya hii narration yote ni kueleza kuwa kila zama na kitabu chake...enzi ikienda hairudi tena. Kitu ambacho ni common ni kuwa tamaduni mbalimbali za tawala zilizotangulia zilirithiwa na tawala zilizofutia.

Timeline ya tawala za dunia hadi mwisho wa dunia hii Mungu alifunua kupitia ndoto aliyomwotesha mfalme Nebukadneza iliyofasiriwa na nabii Daniel na maono aliyoyaona Daniel kuhusiana na wale wanyama wanne.

So ile Greece supremacy haiwezi kujirudia till the end...maana utawala wao kama malaika Gabriel alivyomuelekeza Daniel ulikuja kama ulivyotabiriwa na ukapita wakaja wengine.
 
Waarabu walianzisha hesabu za aljebra
Ku a muda natamani tukae tupige historia za Mesopotamia, Misri, Israel,Norway, Greece, basi tu hua Napenda sana masuala ya historia na deity mbalimbali...
Ila misri kwakua ni hapahapa Afrika napenda Zaid.

wakati mfamle Themistocles wa Jiji la Athens (Ugirki) anahangaika kuhamasisha wafalme wa majiji mengine kama Queen Gogo, King Leonidas waungane wawe taifa moja wao wamisri walikua wanafanya vumbuzi kubwa kubwa zilizoacha ulimwengu kinywa wazi. Nitaorodhesha baadhi ya mambo machache ambayo yamegunduliwa na wamisri weusi kipindi hiko hata Amerika kunakaa nyani na sokwe ,Red Indian na Wamaya

Baadhi ya vitu vilivyogunduiwa na wamisri

Mathematics
Wakati wanasayansi kutoka ugiriki kama Euclid,Pythogras,Archimedes na ugiriki kwa ujumla wakipewa heshima ya kuvumbua hisabati lakini ukweli mchungu ni kwamba wamisri ndio wamegundua hisabati. Geometry,survey,vyote hvyo vimegunduliwa Misri.

Maandishi
Wamisri ndio waliogundua mfumo wa kuweka lugha yao katika maandishi, walikua na mfumo wao wa maandishi unaitwa pictograms, kutokana na picha hizo ndipo kulipozaliwa herufi mbalimbali lakini hii iliendelezwa zaidi na wagiriki’

Dawa ya meno
Kama meno yako ni meupe na masafi basi nenda katambikie kuheshimu mizimu ya mababu zenu wa kimisri maana bila wao tusingepata dawa ya meno.

Wigi, Make-Up na Vipodozi
Mnasikia kua mwanamke mzuri zaidi duniani ni Cleopatra, basi uzuri wake ulichagizwa na vipodozi na make ups za kutosha. Wewe dada waheshimu sana wamisri maana bila wao sijui ingekuaje, miaka hiyo hata Yakobo hajahamia misri..watu wa misri walikua washagundua kuvaa mawigi,kutengeneza vipodozi na kufanya make up. Wanja na kuchonga nyusi kumeanzia huko misri, mafarao ilikua sifa kwao kupaka wanja na make up..nyusi wananyoa zote. Ikumbukwe kwamba wamisri walikua hawapaki wanja kama urembo ila ilikua ni kwa ajili ya imani zao pia waliamini kufanyia macho urembo kulikua kunawasaidia kuwakinga na magonjwa ya macho.

Wino Mweusi, Karatasi na Meza
Juhudi za watu weusi ndio zinafanya wazungu waweze kukaa na kuandika propaganda zao kuhusu watu weusi.wamisri ndio wamegundua wino mweusi kwa ajili ya kuandikia na kutengeneza meza. Wakati wazungu na watu wa jamii zingine wakitumia mbao,mawe na ngozi katika kuandika Wao wamisri walivumbua Karatasi za kuandikia zilikua zinaitwa “papylus sheets”. Baadae wagiriki waliziboresha na kuziita paper kutokana na neno Papyrus.

Mashine za kuvuna na kusaga nafaka na kilimo cha umwagiliaji
Wao ndio walivumbua mashine za kuvuna na kusaga/kukoboa nafaka hasa ngano, miaka hii Israel ndio inasifika kwa kilimo cha umwagiliaji na kua sehemu ya tafiti za kilimo cha umwagiliaji duniani lakini ukweli ni kwamba misri ya kale ndio ilianza kugunda kilimo cha umwagiliaji. Wamisr wa kale walijenga mifereji mingi kusambaza maji kutoka mto nile kupeleka mashambani.

Majira na Kalenda
Wakati red Indians wa marekani wakiokota matunda nan a kuwinda wadudu kama mlo wa siku kwenye misitu mikubwa iliyokuwepo Newyork miaka ya 1300AD, Miaka karibia elfu kadhaa iliyopita kabla ya Kristo wazee wa Afrika kutoka misri walikua wameshagundua jinsi ya kutambua saa za siku na kutengeneza kalenda ya kuonyesha majira ya mwaka. Kalenda yao ilikua na miezi 12 na siku 365, kila mwezi ulikua na siku 30…lakini pia walikua washatengeneza saa zao za asili ajili ya kupima masaa ya siku.

Kufuli
Wamisri ndio watu wa kwanza kuvumbua kufuli, unambiwa funguo za kufuli zao zilikua zinauweza kua na urefu wa futi 2. Lakini hawa mababu pia sometimes kwenye IT tunawataja kama watu wa kwanza kutengeneza codes, maana ile milango ya Pyramids kuna mingine haifunguliwi na funguo ila ni codes Fulani walizoziweka miaka zaidi ya elfu 5 iliyopita. Hivyo hata coding tunaweza sema imeanzia misri.

Polisi na Serikali
Kama ulikua hujui basi ndio hivyo polisi zimeanzishwa kwa mara ya kwanza misri, polisi walikua wanatumia siraha na mbwa katika kufanya doria zao. Hakuna maskini wala tajiri aliyekua juu ya sharia halafu adhabu zao ilikua kukupa kichapo, kukuhasi,kukata pua na maskio halafu ukifa ulikua huzikwi unatupwa kama mzoga. Wamisri walikua wanaamini kwamba ukizikwa kwa heshima basi kunauwezekano mkubwa wa kwenda kwenye maisha ya baadae/mbinguni/Afterlife. Mifumo hii ya serikali zetu duniani unazoziona sasa imetengenezwa na wamisri ndio maana Yosef mtoto wa Israel alikua waziri mkuu kipindi kile. Yaani wakati Abrahm Lincoln anatunga definition ya Democracy huko misri wao walikua washamaliza kia kitu kuhusu mifumo-endeshi ya serikali (ujamaa,Udikteta,ubepari nk nk)

Egyptian Hieroglyphics (Aka Emoji za Misri😆)

1629565382879.png

Hii ni michoro adhimu kabisa iliyobuniwa na wazee wa kiafrika ili kuwasiliana, pia zilikua zinatumika kueleza matukio yaliyopita na yajayo..so ilitumika kuweka rekodi za jamii ya watu wa misri. Unaweza kuona mchorouiliochorwa miaka zaidi ya elfu tano iliyopita ukionyesha image ya aeroplane ni ile ie iliyochorwa na Davinci miaka ya 1600sBC
 
Ukifunua vitabu vya sekondari kila definition utaona inaanza "it's greek Word" hata lugha rasmi ya Binomial nomenclature ni Greek tuseme Biology na sayansi kwa ujumla lugha yake ni Kigiriki.

Kwanini?
Asiilimia 70% ya wanafalsafa, Wanasayansi, Wagunduzi wote wanatoka Ugiriki. Kwa ufupi Sayansi imeanzia Misri ya kale na kutapakaa ulaya hasa ugiriki huko ndiko ilikofanyiwa kazi vizuri wewe chunguza kila mwanafalsafa anatoka Ugiriki.

Ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo mia moja ambapo kila mji ulikua na utawala wake, Mji wa Athens na Sparta ndio ilikua miji mikubwa na yenye nguvu zaidi, japo miji hii mra nyingi ilikua inapigana kwa ajili ya kugombania ardhi lakini vilikua vimejiunga pamoja ili kujilinda na uvamizi wa kutoka nje.

Enzi hizo Ugiriki ilikua Ugiriki kweli kuna madume ya haja hasa (Alpha, Beta peoples) mwaka 480 BC Mfalme Leonidas wa Sparta aliongoza jeshi la wanaume 300 tu kupambana na mfalme Xerxes kutoka Persia mwenye jeshi la watu 10000+ lakini waliwachinja hasa richa ya uchache wao. Japo Leonidas aliahindwa ila alijitahidi kuziwia uvamiI huo ambapo baadae Mfalme Xerxes alikuja kuuwawa na mrithi wa leonidas Themistocles

✓✓Kumbuka mfalme Xerxes ndio mfalme aliyemuoa Ester wa kwenye biblia ambae ester alitumia penzi kuziwia kuuwawa kwa Wayahudi wotewaliokua Babeli. (Kaa kumbukumbu zangu zipo sawa) Wafalme wa Persia waliitwa Ahasuerus. (Ahusuhero).

Sasa waku nini kiliwapata hawa watu? Gunduzi zote zilizofanywa kwao haziwanufaishi. Nilitegemea Ugiriki iwe miongoni mwa Super power county ila hata G7 haipo sijui G20.

Nini kiliwatokea? Sasa hivi hamna tena watu wenye akili au??
mzee napenda sana mada zako
 
Hawa Wagiriki si ndio Wayunani? Hawa walijaliwa kuwa na Elimu na Maarifa ya dunia na Mungu mwenyewe, Waliangushwa na Warumi ambao wao walitabiriwa kushika Elimu na Uchumi (chuma & Udongo) wa dunia mpaka hivi leo.
 
Waarabu waligundua namba, na muda. Katika tiba Waarabu wameleta mabadiliko makubwa katika matumizi ya opium kumfanya mtu alale na tiba iendelee.
actually romour has it arabic numerals were inveted in India by Hindus... Pia kumbuka ingawa hizi arabic numerals ni superior huko western walikuwa wanatumia roman numerals kabla ya kuamia kwenye hizi namba ambazo ni bora zaidi 1, 2, 3, 4....

What we call Arabic numeralsOffsite Link were invented in India by the Hindus. Because the Arabs transmitted this system to the West after the Hindu numerical system found its way to Persia, the numeral system became known as Arabic numerals
 
Mzee baba ulitakiwa kuwalaumu waafrika maana hao wagiriki ni chamtoto kabsa, technologia yote na theories zote za kisayansi walizowakalilisha walimu wenu wa uongo ni copied from ancients Africans, yaan karbia 90% ya sayans na technologia zlianzia afrika zkaja ugiriki, then kwa waarabu&wahind&wachina na watu wamwisho ni warumi au wazungu wotee.

na ndvyo ilivyo, mm nna ushahidi nitajie jambo lolote kubwa unalojua kavumbua mgiriki au mrumi kama halina mkono wa muafrika nyuma, ni vile tulimuhasi MUUMBA wa Afrika, akatupiga laana ya usahaulifu, yaan kila kitu tulchofanya kimesahaulika, kuna baazi ya muvies zmejarbu kuwafungua waafrika kuhusu ukuu wa muafria, lkn sie kwa kukaza akili hatuelewi, mfano kuna muvi ya Avatar ya mwaka 2009 December 19 by james cameron imejarbu kueleza nn kiliikumba jamii kama hii ya black people, pia kuna muvie ya Black panther ya juzi tu hapo nayo imejarbu kwambaal kuonesha ukuu wa muafrika japo kidogo sana lkn vichwa ngumu hamuelewi zaid ya kutizama actions bila kutafakari ujumbe wa muvi hiyo,,

Pia kuna masalia na mabaki ya technology za zaman ambazo mpka leo hii baaz ya watawala wetu wanatuficha kwa kutuhujumu na kuzikabizi kwa mabeberu(JIULIZE KWANINI SAMIA NA KIBARAKA WAKE NDALICHAKO WALISITISHA SOMO LA HISTORIA YA TANZANIA?), pia mujue kuwa hata lile sanduku la agano ambalo ktk biblia zenu za uongo zimelipotosha ukwel wake, ukwel ni kwamba lipo Afrika na linatafutwa zaid ya yanavyotafutwa madini yoyote hapa dunian, na wanaolitafta wanafanya siri, kupitia mawakala wao na maspy wao ambao wanakuja kama watalii, wana dini(catholic), wavumbuz wa mali kale, wawekezaji na mamluki wengine, na hili linafanywa kwa siri sana maana hata waafrika hamtambui hili jambo, na hamuwez kutambua mpka pale akil zetu zitakapoamka kutoka ktk usingiz wa kiroho ambao umesababishwa na sie kushika maadili na imani za hovyo, pia laana ya kumuhasi Muumba wa Dunia ambaye ni zaid ya Uungu wa imani zote za kigen, huyu afananishwi na lolote, hajawai onekana na hatowai onekana kwa kiumbe kama mtu, zaid utahisii uwepo wake kupitia nguvu zake(Roho mtakatifu) Ama nguvu za asiri, ama nature ambayo ina control kila kitu hapa dunian.

Huwa nasikitika sana kuwaona waafrika wanamtukuza mtu mweupe yaani hiyo ni zaid ya kufuru, najua wengi hamjabahatika kupata ukomboz wa fikra ndyomaana bado hamuelewi nachokisema, kila ukionacho hiv leo si kipya, bali kilikuwepo kwa namna nyingine, leo kipo kwa namna nyingne ambayo n namna ya uongo wa kubuni kutoka ktk ukweli halisi....AMKENI WAAFRIKA, WEW NDYE mungu wa dunia baada ya Yule asiefananishwa na lolote, naposema MUUMBA namaanisha zaidi ya Umungu, Muumba wa kwel ni zaid ya umungu wenu mliokalilishwa na imani zakipuuzi hizo....Amkeni wakati ni sasa.
.
IMG-20210612-WA0007.jpg
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
nasikitika kusema kuwa wew bado mchanga ktk elimu ya ugunduzi, na umeshakuwa brainwashed by white supremacy, baazi ya hao uliowataja hawajawai ku exist na hawatowai lakn walifojika kwa kuiba uhusika wa wahusika wakweli na kupachika uhusika wa kwel kwa muhusika wa uongo(imaginary character), na nikikuomba ushahid wao utabaki kujibaraguza hapa maana wew mwenyew umekalil[emoji23][emoji23][emoji23]...wake up bro
 
Back
Top Bottom