Wagombea 20 wapitishwa kugombea Uongozi Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)

Wagombea 20 wapitishwa kugombea Uongozi Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
WAGOMBEA 20 wa nafasi za uongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), uchaguzi unaotarajia kufanyika Desemba 14, 2024 Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Kamati ya Uchaguzi wa TOC, Ibrahim Mkwawa waliopitishwa kwa Urais ni Michael Washa, Anthony Mtaka, Henry Tandau na Nasra Juma Mohamed huku wanaowania nafasi Makamu wa Rais ni Suleiman Mahmoud Jabir na Jamal Nassor Adi.

Wanaowania Kamati ya Utendaji (Tanzania bara) ni Muharram Mchume, Lwiza John, Godfrey Mhagama, Fatma Yassoda, Suma Mwaitenda, David Mwasyoge, Devotha Marwa, Alfredo Shahanga, Adolfina Mohamed, Khalid Rushaka, Noorelain Sharrif na Donald Masawe.

Kwa upande wa Zanzibar walioomba nafasi hiyo ni Kassim Hussein Saleh, Faida Salmin Juma, Mwatima Bakari Abdi, Makame Ali Machano, Said Mohamed Abdulla, Juma Khamis Zaidi, Suleiman Ame Khamis na AbdulRahman Said Simai.

Aidha, Mkwawa alisema siku tatu hizi ni kipindi cha pingamizi kwa wagombea hao.
 
Back
Top Bottom