johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 104,319
- 183,639
Ndio....Kwani CDM kitakuwa na wabunge?
Mpaka unatoa ushauri huo,kwani watapata mbunge hata mmoja safari hii?Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.
Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.
Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.
Maendeleo hayana vyama!
Siasa ni sayansi komredi!Mpaka unatoa ushauri huo,kwani watapata mbunge hata mmoja safari hii?
Kwa hiyo wanaweza kutumia sayansi wakapindua meza? Sio Chadema hii.Siasa ni sayansi komredi!
Mwambieni huyo anayewaghilibu na kuliingiza Taifa hasara ya kurudia uchaguzi.Natoa angalizo na nina imani Mbowe na Mnyika mnanisikia popote mlipo.
Ni kwamba kulikoni kutuletea sintofahamu katikati ya muhula ni bora hawa wagombea wenu wa Ubunge mkawalisha yamini au kiapo ili wasituache kwenye mataa katikati ya muhula na kukimbilia CCM.
Tumechoka na habari ya kumchagua Mbunge huyo huyo mara mbili kama ilivyokuwa kwa Mwita Waitara.
Maendeleo hayana vyama!
Hahahaaaa...... Mimi nasubiri muziki wa Pierre Liquid na mchungaji Msigwa!Kwa hiyo wanaweza kutumia sayansi wakapindua meza? Sio Chadema hii.
Mpaka unatoa ushauri huo,kwani watapata mbunge hata mmoja safari hii?
Tume haihusiki. Wananchi hawataki kuisikia Chadema. Imechafuka kabisa ni matapeli wa kisiasa.Kwani Magufuli ameagiza tume isiyo huru ya uchaguzi, iwape Cdm viti vingapi vya ubunge?
Tume haihusiki. Wananchi hawataki kuisikia Chadema. Imechafuka kabisa ni matapeli wa kisiasa.
Uzuri kila kitu hufanyika kwa uwazi na kila chama huwa na mawakala na hutakiwa kulinda kura za chama chao. Pia mawakala huwa wanajaza fomu zote zinazotakiwa na matokeo hupandikwa kwenye kila kituo ngazi zote. Kwa hiyo propaganda zako ni uswahili usio na mbele wala nyuma.Ushenzi, uhayawani na ukatili wa wazi unaofanyika kwenye chaguzi zetu ili ccm watangazwe washindi, hakuna mtanzania asiyeujua. Tunafahamu kila kitu na wala hatuhadithiwi.
Uzuri kila kitu hufanyika kwa uwazi na kila chama huwa na mawakala na hutakiwa kulinda kura za chama chao. Pia mawakala huwa wanajaza fomu zote zinazotakiwa na matokeo hupandikwa kwenye kila kituo ngazi zote. Kwa hiyo propaganda zako ni uswahili usio na mbele wala nyuma.
Maneno ya mshindwaji.Sina chembe ya shaka na nilichokisema. Huo uhuni, ukatali na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi, umefanyika mbele ya macho yangu na wapiga kura wengine. Tena umefanyika kwa uratibu wa vyombo vya dola, na tume isiyo huru ya uchaguzi. Hii ndio sababu watu wengi kudharau box la kura, kwa kiwango cha hali ya juu toka nchi hii ipate uhuru.
Mimi mpaka leo bado nashangaa watu wazima na sharubu zao kulia na kalalamika kuwa wanarubuniwa. Sijui wakati wanarubuniwa wenyewe wanakuwa wapi 🤷♂️CCM waache tabia hii ya kuwarubuni hawa watu, Rushwa ni adui wa Haki, sintatoa wala kupokea rushwa.