Msongoru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 306
- 24
na Anna Makange, Tanga
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya wagombea wake wawili waliokuwa wakiwania udiwani katika Kata ya Ngamiani Kati na Chongoleani, wilayani hapa kubwagwa kwenye uchaguzi mdogo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, Chama cha Wananchi (CUF) kilipata ushindi kwa wagombea wake kuongoza katika kata zote mbili.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana kuhusiana na uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Tanga, Paul Baruti, alisema mgombea aliyeshinda ni Nabahan Habib wa CUF aliyepata kura 634, akifuatiwa na Mohamed Thabit wa CCM aliyepata kura 391 na Aziz Mahadh wa CHADEMA aliyepata kura 112.
Alisema waliokuwa wamejiandkisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Ngamiani Kati ni watu 4,070, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 1,145 wakati kura halali zilikuwa 1,138 na saba ziliharibika.
Kwa upande wa Kata ya Chongoleani alisema mgombea Ali Ng'anzi wa CUF alishinda kwa kupata kura 567 kati ya kura halali 1,121 zilizopigwa na kumshinda Hamis Jasho wa CCM aliyepata kura 454.
Uchaguzi huo mdogo umefanyika ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na aliyekuwa diwani wa Ngamiani Kati, Salimu Akida (CUF) aliyehamia nchini Marekani mwaka 2006.
Uchaguzi katika Kata ya Chongoleani ulifanyika baada