Viongozi wengi wa Urais hasa wa Ki Afrika tamaa yao kubwa ni kuona wanapata madaraka makubwa kwa kipindi kifupi cha lala salama kabla ya uchaguzi pasipo kuyaishi maisha ya wananchi wanaotaka kuwaongoza.
Kipindi hiki cha uchaguzi tutashuhudia viongozi wengi wakipitapita mitaani, wengine wakiwapigia magoti watoto wao wa kuzaa kwa ajili ya kura, ndicho kipindi cha kuwaona wakila kwa mama ntilie, wakikaa kwenye vumbi na matope, wakichimba mitaro wengine wakijifanya mafundi washi n.k. Walikwina?
Miaka mitano wameshuhudia wapinzani wakipata misukosuko, kina Zitto wakiwekwa ndani, Mbowe akivunjwa miguu, Lissu akipigwa risasi, Seifu akidhulumiwa chama chake, wakati huo wao wanakula bata na wadhulumati, hatukuwasikia, kumbuka anayenyamaza wakati maonevu yakitendeka naye yuko upande wao.
Lowassa aliingia Chadema dakika za lala salama na kuteuliwa kugombea urais bila kuangalia ni jinsi gani waliojitolea maisha yao kina Mawazo walivyopata matatizo kukijenga chama.
Membe naye nimemsikia anataka kugombea upinzani hasa ACT Wazalendo, anataka kutuambia alikuwa na ACT kiroho ila kimwili alikuwa CCM, hajui Zitto kapata tabu gani kuijenga ACT.
Mimi nasema hapana, kosa si kufanya kosa bali kurudia kosa, wapinzani watakuwa na wenzao kina Seif, Lissu, Mbowe walioumia nao kimwili, wao wapambane huko huko CCM waliokuwa nao kimwili.
Kama ilivyokuwa kwa Lowassa Membe akikosa alichokuwa anatamani atarudi alikotoka.