Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 866
Wakuu
Nimeona ni vema niwaletee swali la Msingi la Mhonga Said (MB) VIti Maalum CHADEMA alilouliza kwenye Bunge Nov 4 Mwaka huu. Akitaka kufahamu yafuatayo na Jibu alilopewa na Waziri.
Jamani hivi kweli hii ni sahihi,kung'an'gania Katiba, Katiba,Kwani Katiba ni kitu gani mpaka isibadilishwe,Hivi CCM wanadhani watakuwa madarakani milele?
Swali lilikuwa kama ifuatavyo:
Kwa kuwa Serikali ina mpango wa kuleta mabadiliko na Sheria ya Uchaguzi kufuatia taarifa iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu katika hotuba yake ya Bajeti; kawa kuwa Bunge ndiyo chombo kikuu kinachotunga Sheria na kuamua juu ya mustakabali wa maisha ya Watanzania:-
(a) Je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kuweka kifungu kinachoruhusu wagombea Urais wote watakaopata asilimia tatu hadi tano ya kura za Urais kuwa wawakilishi ndani ya Bunge kama nchi nyingine ili kutimiza matakwa ya demokrasia?
(b) Je , Serikali haioni kuwa Sheria hiyo ikiwaruhusu wagombea Urais hao kuwa wawakilishi itasaidia kuchangia mawazo katika yale yaliyowasukuma kugombea nafasi hiyo?
Na haya ndio Majibu ya Waziri Marmo Phillip
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali ina mpango wa kuleta Bungeni mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi. Mapendekezo ya Marekebisho hayo ya Sheria ya Uchaguzi yana lengo la kuondoa kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na chaguzi ndogo zilizofanyika baada ya Uchaguzi Mkuu huo. Madhumuni makubwa ya marekebisho hayo ni kuiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendesha mchakato wa uchaguzi kwa wepesi na ufanisi zaidi hasa kwa kuwa Sheria za uchaguzi zinahusu zaidi mambo ya mchakato wa uchaguzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuweka kifungu kinachoruhusu wagombea Urais wote watakaopata asilimia tatu hadi tano ya kura za Urais kuwa wawakilishi ndani ya Bunge ni suala la Kikatiba. Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inatamka bayana aina ya Wabunge na sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano.Namshauri Mheshimiwa Mbunge kukubali wagombea wajiimarishe kuwania ushindi na siyo kulenga kuwa wawakilishi wa vyama Bungeni kwa kuwa washindi wateule watakuwa wamepatikana na kujaza nafasi zote kwa mujibu wa Katiba.
Wakuu hebu tuajdili haya majibu yanaridhisha kweli?hayajakaa kukuandamizi na kbaka demokarsia kweli?hivi je kweli Tanzania ni democratic country?mbona upinzani uanakandamizwa sana?