Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Mara nyingi nimesema sana humu JF kwamba kuna wakati nazishangaa sana kauli za wanasiasa wetu zinazotolewa kama vile hawana uwezo wa kufikiri. Sasa hili la Bashiru, Katibu Mkuu wa CCM kupiga kelele mbele ya jumuiya kwamba haelewi kwa nini hadi wakati huo wanachama 12 wajitokeze kugombea uraisi Zanzibar ni mojawapo ya kauli potofu sana kufanywa na kiongozi wa juu wa kisiasa kwa sababu zifuatazo;
Think before you talk.
- Kauli ya Bashiru inaashiria kuwa tayari CCM wana mtu wao ambae "ameshateuliwa" na huyo peke yake ndie anapaswa kuchukua form za uraisi wa Zanzibar
- Kauli ya Bashiru ni wonyesho wazi kwamba ndani ya CCM hawajali demokrasia wala kufuata katiba yao wenyewe, viongozi wa juu waliopo madarakani ndio wanaamua nani apewe uongozi wengine wote hawatasikilizwa
- Kauli ya Bashiru ina maana kwamba isipkuwa mtu mmoja, wengine wote waliochukua form za Uraisi Zanzibar wanatumiwa na "mabeberu" na CCM inajua hilo japo imewaacha waendelee kuwa katika nafasi zao katika chama
- Kwamba kama wewe sio mtu wa kundi la "CCM ya wenyewe" basi ndani ya CCM hata ufanyeje hutafanikiwa, na kugombea nafasi za uongozi ni kujipotezea muda
Think before you talk.