Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Wagombea wa CCM waweza kushinda bila ya uharamia na mchezo mchafu?
Imekuwa ni kawaida kwa CCM kwamba kila unapokuja uchaguzi (hata ule wa wao wenyewe ndani (internal party elections) huwa ni ghilba, umafia, uharamia na vitendo vingine vichafu havipaswi hata kuelezea.
Maovu haya yanafanyika katika ngazi zote yaani kuanzia uteuzi wa wagombea wao hadi uchaguzi wenyewe wakishindana na vyama vingine. Jee hii ndiyo imekuwa hulka ya CCM chama ambacho kinaimba wimbo wa kuwa wastaarabu hasa kwa vyama vingine?
Kuna kutishana, hata pengine kutishia mauaji (kama vile vitisho vinavyotolewa na wakala wao mkuu Sheikh Yahya Hussein dhidi ya watakaompinga JK).
Hivi sasa tunashuhudia yote haya, huku hatusahau mwaka miaka 5 iliyopita wakati wa uteuzi wa JK. Uharamia uliofanyika wakati ule kumpitisha huyu ulikuwa wa kihistoria kwani ulikigawa chama katika makundi, makundi ambayo yapo hadi leo.
Vyombo vya dola, hasa Intelligence vilitumika kutishia wagombea wengine wajitoe ili kumpitisha Jk ambaye bila ya kufanyika hivyo asingefua dafu kwani wengi walikuwa sahihi katika kutabiri kwamba urais wa Jk ungekuwa kituko tu na kweli umekuwa kituko!. Fedha chafu zilitumika fedha ambazo kumbe ziliibwa kutoka BoT.
Swali: Kabisa kabisa CCM haiwezi kiufanya siasa zake kwa njia za kistaarabu?