#COVID19 Wagonjwa 7 waongezeka Uganda, Jumla ya visa yafikia 686. Watanzania 4 na Wakenya 8 warudishwa miongoni mwa waliorudishwa

#COVID19 Wagonjwa 7 waongezeka Uganda, Jumla ya visa yafikia 686. Watanzania 4 na Wakenya 8 warudishwa miongoni mwa waliorudishwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Wizara ya Afya imetangaza Wagonjwa wapya 07 wa #COVID19 baada ya sampuli 2,532 kupimwa jana. Wagonjwa wote ni Waganda na jumla ya maambukizi imefikia 686

Wagonjwa 3 wamepatika katika sampuli 1,310 zilizopimwa mipakani na Wagonjwa 4 wamepatikana katika sampuli 1,164 zilizopimwa kutoka kwa watu walionesha dalili au waliokutana na Wagonjwa. Sampuli 58 za Wafanyakazi wa afya zimeonesha hazina maambukizi

Waliopatikana mipakani wamepatikana katika mipaka ya Malaba (2) na Mutukula (1) huku wanne waliobaki wametokea Wilaya ya Tororo (2), Wilaya ya Kyotera (1) na Wilaya ya Gulu (1)

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki imetangaza jumla ya Wagonjwa 161 waliopona na hakuna kifo hadi sasa

Aidha, Wizara imetangaza Madereva 18 waliozuiliwa kuingia Uganda na kurudishwa nchini mwao baada ya kukutwa na COVID19. Madereva hao wanatoka Kenya (8), Tanzania (4), Congo (2), Sudan Kusini (2) na Eritrea (2)

EaS_oTRXQAIi30j.jpg
 
Back
Top Bottom