MwakiIV
Member
- Aug 31, 2018
- 79
- 138
Siku ya leo 17/03/2023
Kuna ajali imetokea asubuhi ya leo ambayo imesababisha majeruhi wawili, majeruhi hao walipata huduma ya kwanza kwenye Zahanati ya Kigamboni na baadae tupewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke.
Baada ya kupokelewa ukawa na changamoto ya Umeme ambapo hata Jenereta lililopo hapa limeshindwa kuwaka hivyo kupelekea huduma kusimama kwa zaidi ya masaa 3.
Wagonjwa waliendelea kuja kwa wingi, lakini mfumo wa hospitali haukuwa unafanya kazi kuanzia kwenyeusajili, malipo, vipimo na matibabu.
Hivyo waudumu na madaktari ni kama walikuwa wanazurura tu.
SWALI:
1. Kitu kinachoitwa mfumo ni suala la upeo wa binadamu kwa nini hakuna njia mbadala ya mfumo endapo digitali ikafeli?
2. Hadhi ya hii hospitali inakosaje jenereta la kuwezesha huduma zikaendelea?