#COVID19 Wagonjwa wapya 30 waongezeka. Visa vyafikia 646. Madereva 43 wa Kenya na 4 wa Tanzania warudishwa baada ya kukutwa na maambukizi

#COVID19 Wagonjwa wapya 30 waongezeka. Visa vyafikia 646. Madereva 43 wa Kenya na 4 wa Tanzania warudishwa baada ya kukutwa na maambukizi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Wizara ya Afya nchini humo imetangaza ongezeko la Wagonjwa 30 baada ya sampuli 3,758 kufanyiwa vipimo kwa siku ya jana. Idadi ya maambukizi nchini humo imefikia 646

Katika sampuli hizo 3,758, sampuli 1,876 zilipimwa mipakani, sampuli 1,728 zilipimwa kwa Watu waliokuwa wakifuatiliwa baada ya kukutana na wenye maambukizi huku sampuli 154 zikipimwa kwa Wafanyakazi wa Afya

Katika Wagonjwa wapya 30, Wagonjwa 4 ni madereva wa Malori walioingia #Uganda kutokea Sudan Kusini kupitia mpaka wa Elegu, na mmoja ni dereva wa lori aliyetokea Kenya na kuingia Uganda kupitia mpaka wa Busia

Wengine wanne ni Wafanyakazi wa Afya ambapo sasa jumla ya Wafanyakazi wa Afya 22 wamekutwa na #CoronaVirus nchini humo. Pia, wengine watatu ni Watu wa Ulinzi katika Wilaya ya Luwero

Pamoja na hao, Wagonjwa 18 ni wale waliokutana na watu waliokuwa na maambukizi ambapo 18 hao wanatokea Amuru (4), Tororo (3), Buikwe (3), Kyankwanzi (2), Arua (2) pamoja na Buliisa, Wakiso, Kisoro na Kampala kukiwa na mgonjwa mmoja mmoja

Nchi ambayo hadi sasa haina kifo cha mgonjwa wa #COVID19 imeripoti jumla ya Wagonjwa 103 waliopona

Aidha, Madereva wengine 51 wamerudishwa nchini mwao baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo. Madereva hao wanatoka; Kenya (43), Tanzania (4), Burundi (3) na mmoja anatoka Eritrea

photo_2020-06-08_13-39-06.jpg
 
Back
Top Bottom