Wagonjwa wenye matatizo ya akili watoroka hospitali

KWEZISHO

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2016
Posts
7,519
Reaction score
6,518
Wagonjwa kadha wenye matatizo ya kiakili wameitoroka hospitali kuu ya wagonjwa wenye matatizo ya kiakili nchini Kenya, hospitali ya Mathari jijini Nairobi.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema huenda wagonjwa hao wametumia fursa ya kutokuwepo kwa madaktari wanaogoma kutoroka.

Polisi wanawasaka wagonjwa hao.

Gazeti la Nation linasema wagonjwa waliotoroka ni karibu 50 ingawa Standard linaripoti kwamba huenda wakafikia 100.

Madaktari na wauguzi kote nchini Kenya wanagoma kuishinikiza serikali iwalipe malimbikizi ya nyongeza ya mishahara na marupurupu mengine chini ya makubaliano yaliyotiwa saini Juni mwaka 2013.

Mgomo huo umeathiri hospitali zote zinazoendeshwa na serikali za majimbo pamoja na hospitali kuu za rufaa - Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Hospitali ya Moi mjini Eldoret.

Maafisa wakuu wa afya serikali walifanya mkutano wa dharura Jumapili usiku kujaribu kuzuia mgomo huo lakini juhudi zao hazikufua dafu.

Chanzo: BBC Swahili

My take: Wakati mwingine unapoongea na wakenya uwe muangalifu sana. Yawezekana ni mmoja kati ya hawa.
 
m nawasifu kenya wameadvance sana katika suala la kuweka wagonjwa wa akili na huduma za hospitali.....jamani wenzangu tunaoisifia kenya kila jambo njooni
 
m nawasifu kenya wameadvance sana katika suala la kuweka wagonjwa wa akili na huduma za hospitali.....jamani wenzangu tunaoisifia kenya kila jambo njooni
Mzee isije ikawa unawaalika miongoni mwa hao watoro!
 
Ooh kuna mmoja kachangia kwenye post yangu inayomhusu Omondi nikajua tu moja kwa moja huyu ni case
 
m nawasifu kenya wameadvance sana katika suala la kuweka wagonjwa wa akili na huduma za hospitali.....jamani wenzangu tunaoisifia kenya kila jambo njooni
Kenyan teachers are now the third highest paid teachers in africa after morroccan and south afican Teachers in afew months when a kenyan doctor is earning more than a Tanzanian MP come and tell me what you think

View attachment 442976
Mp wa tz analipwa tsh ngapi?
doctor wa Kenya analipwa tsh ngapi?
 
PRESIDENT UHURU KENYATTA..JUST GIVE DR MATIANG'I A CALL and let him run all ministries in KENYA...
 
Mh kweli hawa ni vichaa, hizo wanazopanda juu sio fensi ya umeme kweli? Madaktari naona wameamua kuonyesha kwamba walienda shule kusoma na wanajua kazi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…