Wagosi wa Kaya popote mlipo, nawapa maua yenu albamu iitwayo "UKWELI MTUPU"

Wagosi wa Kaya popote mlipo, nawapa maua yenu albamu iitwayo "UKWELI MTUPU"

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (75)✍️
Februari 24, 2002 ilizinduliwa albamu iitwayo "UKWELI MTUPU" kutoka kwa wasanii wawili, si wengine bali ni WAGOSI WA KAYA kutokea kule mtaa wa Kisosora, Tanga mjini. Mmoja aliimba kwa lafudhi ya Kidigo, na mwingine aliimba kwa lafudhi ya Kisambaa.

Ilikuwa ni albamu iliyosheheni nyimbo nane (8) zilizobeba jumbe mbalimbali. Ni nyimbo ambazo unaweza kusikiliza popote na mbele ya mtu yeyote awe mtoto, mzazi, mkwe, muumini, au mwingine yeyote.

Zifuatazo ni nyimbo zilizopo kwenye albamu hii.
1. Tanga Kunani.
2. Wauguzi.
3. Tutamtambuaje.
4. Wakulima.
5. Vinatia uchungu.
6. Mnajua nampenda.
7. Kero (umeme na maji).
8. Tanga kunani remix.

Licha ya nyimbo za aina hiyo kuwa na jumbe nzuri kwa serikali na jamii; lakini hazikuwapatia pesa nyingi wasanii, hivyo kusababisha wasanii hao kupotea taratibu kwenye tasnia ya muziki. Ndipo waliibuka wasanii wa nyimbo za matusi, uchi uchi, na ushenyentwa-ushenyentwa.

💐Wagosi wa Kaya popote mlipo, nawapa maua yenu.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM.
 

Attachments

  • Screenshot_20250103-234716.jpg
    Screenshot_20250103-234716.jpg
    190 KB · Views: 6
Ayaaa aaaaa traffic huyooo....ngoja nijaribu Kama tutapitaa....😊😊😊

Enzi izo walikua wanapiga masuruali makubwaa...siku wameenda mj records first time... masters j aliwashangaaa.. akasema kimoyo moyo Hawa ma DINGI wataweza kuimba/ ku rap 😁😁

The remaining is history moja ya kundi lililo shawishi wazee waamini kua MZIKI SIO UHUNI
 
Back
Top Bottom