Wahabeshi 47 wafungwa miezi sita jela

Wahabeshi 47 wafungwa miezi sita jela

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Tanga. Hatimaye, wahamiaji haramu 47 wa Ethiopia waliokamatwa wakiwa wanasafirishwa ndani ya makontena, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kuishi nchini isivyo halali.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde,baada ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani kwamara ya pili, kufuatia kupatikana kwa mkalimani wa lugha ya kwao.

Kabla ya hukumu hiyo, Mwanasheria wa Idara ya Uhamiaji mkoani Tanga, Adam Kinyamagoha, alidai kuwa washtakiwa walikamatwa Machi Mosi mwaka huu katika Kijiji cha Kitumbi, wilayani Handeni. Alidai kwamba watu hao walikamatwa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani baada ya kuyasimamisha malori aina ya Scania yanamilikiwa na Kampuni ya Charan Sigh $ Sons Ltd na kusikia kelele za kugongwa kwa makontena yaliyokuwa yakisafirishwa na malori hayo.

Alisema ‘baadaye ofisa huyo wa polisi aliamuru yafunguliwe.”
Hakimu Maira aliwataka ama kulipa faini ya Sh50,000 kila mmoja au kwenda jela miezi sita.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1726640/-/128pux8/-/index.html
 
UHAMIAJI.jpg
 
Wangewarudisha kwao tu ghalama za kuwatunza ni kubwa
 
mmiliki wa hilo gari lililo kuwa likiwasafirisha hao wahabeshi alitakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ambazo ni kali zaidi kuliko hata hao wahamiaji haramu.
 
Serikali ilichotakiwa kufanya ni kutaifisha hilo gari lililobeba hao watu sio kuwafunga na kumuachia mwenye gari aendelee na biashara ya kusafirisha watu. Akili ndogo kutawala akili kubwa ndio tatizo lake
 
1.Serikali ifanye makubaliano na serikali zao kwamba serikali zao zitalipa nauli za ndege kuwarudisha wahamiaji haramu kwao.

2.Kuwaweka mahabusu/ gerezani ni gharama mno kwa serikali.

3.Serikali Ifanye deal na UNHCR wagharamie gharama za kuwaweka kambini

4. Serikali itambue kuwa hii ni biashara kubwa duniani na wasipokuwa waangalifu nchii itajaa wahamiaji na hakuna dalili yeyote ya kupungua kwa wimbi la migration. So long as there will be problems in other countries (problems which we dont have control over them) whether economical, political or social - we are guaranteed to continually having migrants from all over the world.

We need to deal with it.
 
Back
Top Bottom