Mkomawatu
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 273
- 123
Hakika ni dhairi isiyo kificho kuwa vyuo vikuu sehemu yeyote duniani zimekuwa kama chemchem ya kuzalisha vijana katika taaluma mbalimbali ambao baadae wengi wao huwa watumishi wa umma na hata viongozi wa ngazi za juu serikalini,tunayo mifano mbalimbali ya wahadhiri ambao mawazo yao chanya waliyoyatoa kwa vijana vyuo vikuu na pia kupitia makongamano na maandiko yao vilipelekea jamii zao kujikomboa kisiasa,kiuchumi na hata kijamii,mfano mzuri ni mwandishi nguli wa kenya Profesa Ngugi wa Thiong'o,Profesa Wamba Dia Wamba wa Congo DRC, hawa kazi zao zilipelekea kutishiwa maisha na watawala wao hadi kukimbilia ughaibuni,bila kumsahau mwanazuoni kipenzi cha wengi hayati Walter Rodney ambaye alifundisha Chuo kikuu cha Daressalaam miaka ya sitini hadi sabini,Rodney aliuwawa na Serikali ya Guyana kutokana na mawazo yake ya kimapinduzi,hali hii ni tofauti na nchini kwetu Tanzania ambapo vyuo vikuu vimegeuka sehemu ya kuogopeka kuusema ukweli na hata kupinga ukandamizaji,yaani vijana wanaishi kwa unyenyekevu kama wapo madhabauni au waumini msikitini wakimsikiliza imam akitoa hotuba katika mimbari,wakati huo huo tunashuhudia wahadhiri wao wakitoa tafiti na makala za ujanja ujanja kuwasafisha watawala na hata kuwaandalia ilani za uchaguzi,jambo hili linasikitisha na kuhuzunisha sana,ifike mahali wafuate nyayo za wenzao akina hayati Profesa Seith Chachage na mwenzake Haroub Othman hawa waliamini katika ulimwengu wa ukweli na si "undumilakuwili". Tanzania yenye neema italetwa na mimi,wewe na yule.