Wahadhiri wa Vyuo Vikuu na mishahara ya Wabunge na Wakurugenzi Mashirika ya Umma

Wangekuwa wanalipwa vzr wasingebuni vikai vya ajabu ajabu ili wapate posho.
 
Nchi zilizoendelea maprofesa wanajikita katika taaluma zao kwa manufaa ya Taifa, ila nchi masikini maprofesa wanakimbilia kwenye siasa, imekaaje?
 
Ushauri wako mzuri Sana lkn wanaopaswa kulifanyia kazi wazo lako ndiyo hao hao akina msukuma na kibajaji ambao kila kukicha wanaiponda elimu ndani ya bunge. Unategemea mwitikio chanya ktk hili??
 
Wangekuwa wanalipwa vzr wasingebuni vikai vya ajabu ajabu ili wapate posho.
Hiyo haiwezi kuwa excuse! Unaweza kushangaa chuo kikuu kisicho cha umma kama SAUT (wajenge majengo, walipe mishahara, walipe gharama za uendeshaji wa chuo za kila siku, umeme, maji, usafi, n.k) kupitia ada za wanafunzi na mambo yao yanakwenda.

Linganisha Chuo cha umma ambapo majengo yote serikali,,gharama za uendeshaji serikali, wanafunzi wengi wanaenda vyuo vya umma maana yake ada ya kutosha, magari serikali, mishahara ya walimu na wafanyakazi waendeshaji serikali.

Lakini linapokuja suala la impact hakuna tofauti kati ya chuo cha private kama Saut chenye resources chache na vyuo vya umma vyenye support ya serikali asilimia 100.

Huo si upuuzi tu.
 
Yaani utakuta mtu hana hata ubongo wowote, lkn kwa sababu anajua kubwabwaja na figisu, basi tayari anakuws mwana siasa, baadaye mbunge. Huu ni ujinga ulioje!!
Hii ni nchi ya figisu, fitina na kujipendekeza ili mradi tu mkono uende kinywani
 
Duuh!

Ila hata JF ni think tank ki-dizaini.
 
LOGIC
 
Yani inashangaza sana mtu ana PhD anapata mshahara hawezi hata ku afford a comfortable life. Wengi wana stress sana vyuoni. Wanafanyakazi siku ziende wapate wanachopa.

Serikali ufanye uchunguzi tu, wengi wana stress na depression.
 
Moja ya sifa kubwa ya nchi zinazoendelea (maskini) ni kutojali elimu.

Zitamlipa mamilioni jamaa fulani anayeenda kusema kuwa daraja la pale kata ya mjimwema ni la muhimu (wakati mkuu wa wilaya, mkoa, madiwani wanajua na wanaweza fikisha habari) halafu litamlipa vijisenti jamaa anayekwenda kutoa maarifa jinsi ya kulitengeneza.

Kwa mwendo huu tutajengewa na kutengenezewa sana vitu vyetu na wazungu na wachina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…