Wahadhiri Wagoma Tena UDOM!

Mdau

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2008
Posts
1,789
Reaction score
473
Wadau,taarifa confirmed toka Dodoma zinasema kwamba leo wahadhiri wamegoma tena baada ya kuambiwa kwamba mishahara watakayopokea mwezi huu haitakua na mabadiliko yeyote tofauti na walivyoahidiwa na Pinda....mwenye maelezo zaidi atuletee tafadhali...
 
man hujaandika source umepata wapi?nadhani ingeturahisishia sana tuanzie wapi kuuliza
Wadau,taarifa confirmed toka Dodoma zinasema kwamba leo wahadhiri wamegoma tena baada ya kuambiwa kwamba mishahara watakayopokea mwezi huu haitakua na mabadiliko yeyote tofauti na walivyoahidiwa na Pinda....mwenye maelezo zaidi atuletee tafadhali...
 
Breaking news si lazima ziwe na reliable source. Nami pia nimezipata na source yangu ni mwanagu anaesoma pale. Nahisi hii ni virus kama wale wa Tunisia na Misri, kaingia UDOM na anaweza kusambaa pande yoyote ndani ya nchi hii kwani kote kuna mazingira rafiki ya kirusi kuishi na ku-multiply.
 

Kuna mtu kaniambia redi fulani imetangaza. Lakini pia, naambiwa kuwa mgomo huo umeahirishwa.
 
Aisee basi ngoja nicheki na jamaa zangu wanafundisha pale may be nitapata information zaidi!hii hali ni hatari sasa hivi shule za kukatakata mitaala inamalizwa kweli maana huwa sioni kama wanaongeza muda wa msomo kufidia hizi siku za migomo na kama hawaongezi maana yake wanafunzi wanapunjwa muda wao wa kuwa darasani ma matokeo yake ndiyo hayo mwanafunzi anamaliza degree lakini anakua na degree jina kichwani hakuna kitu hv hili wahusika hawalioni!
Employee wa UDOM kaniambia...
 
:clap2:UDOM hawaja goma jamani, ila kulikuwa na kikao kifupi cha wahadhiri ambacho kilikuwa cha kujadili mambo yanayohusu maslahi yao likiwemo swala la mishahara. Hadi sasa hivi wamesha maliza na kuingia maofisini kama kawa!!!!!!!!!! Ila bado madai yao ya msingi yanaendelea kushughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu!:clap2:
 
Kama sikosei waziri mkuu akisema end of February, sio January!
 
sASA KAMA UNA JAMAA ZAKO PALE SI UNGECHEKI NAO TOKEA AWALI SASA UNAULIZA SOURCE YA NINI ILHALI UNA WATU JIKONI;;ficha upuuzi wako
 
hawajagoma hio ni confirmed nimeongea na rais wa Udomasa na amenihakikishia hamna kitu kama hicho
 
Okey,nikirudi ntakuta taarifa ya maana
 
acha matusi lazima nijue source kwanza ndipo nifanye uchunguzi siwezi anza tu kupiga simu toka mbali bila kujua chanzo utakua ni umbea na naweza ingia gharama bure narudia tena acha dharau tumia busara neno mpuuzi sio lugha nzuri sijalifurahia any way yawezekana ni tabia yako kutokua na busara
sASA KAMA UNA JAMAA ZAKO PALE SI UNGECHEKI NAO TOKEA AWALI SASA UNAULIZA SOURCE YA NINI ILHALI UNA WATU JIKONI;;ficha upuuzi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…