Wahadzabe ni kabila ambalo ni zaidi ya kivutio cha Utalii ila hawapewi kipaumbele kama tunavyowapa Maasai

Wahadzabe ni kabila ambalo ni zaidi ya kivutio cha Utalii ila hawapewi kipaumbele kama tunavyowapa Maasai

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Kusema kweli saiz kabila la kimasai halina maajabu tena ya kufanya tuwape kipaumbele kama kivutio cha watalii kwa kuwa maisha yao ni maisha ya kawaida kabisa, ukiachana na ufugaji wao na uvaaji wao hakuna kingine cha maajabu kinachofanya kutangazwa kama kivutio cha watalii.

Katika filamu ya Mama loyal tower yalifanyika makosa makubwa kama hawakukumbuka kuonesha Dunia maisha ya Wahadzabe,
Lugha zao tamaduni zao na ndoa zao, kusema ukweli Wahadzabe ni zaidi ya kivutio.

Saizi kumetokea wajanja walioijua fulsa na kuichangamkia wanapiga pesa kupitia kuonesha maisha ya kabila hili kupitia mitandao ya kijamii, kama youtube na sehem zingine, na watu wao ambao wamegundua fulsa hii saizi wamejizolea Umaarufu na wafuasi kibao na wafuatiliaje ndani na nje ya Inchi ambao wanafuatilia maisha ya hawa jamaa.

Huku taifa likiwa bado halijagungundua kuwa ipo haja ya kuwekeza nguvu kupromote Tamaduni za watu hawa na kufanya kama chanzo cha utalii wa wawatu kuja kujionea maisha ya Jamii hii ya watu wanaoshangaza.

Na yafuatayo ni miongoni mwa mambo ambayo yanashangaza katika kabila hili.

1. Aina yao ya uwindaji
2. Ndoa zao
3. Vyakula vyao
4. Makazi yao
5. Usafi wao
6. Mavazi yao
7. Mawasliano yao.
8. Ushirikiano wao.
9. Misiba yao.
10. Uongozi wao.

Jamii hii imekuwa iko tofauti kabisa na Maisha ya jamii zote tunazozifaham sisi ila cha ajabu wanaopewa promotion kama vivutio ni Maasai ambao kimsingi hawana maajabu yoyote zaidi ya kuzurula na mavibuyu mikononi na kulinda mageti.

Baada ya kutokea baadhi ya watu kustukia fulsa za kuonesha maisha ya hawa watu kupitia mitandao ya kijamii, Hatmae hii limewafikia Clouds Media na kuwapelekea kuomba mahojiano na vijana wa kabila hili kusema kwel mahojiano hayo yamekuwa na mvuto na watazamaji wengi sana baada ya kushtushwa na maisha ya watu wa jamii hii.

Nataman kama leo tungetumia nguvu kutangaza Kabila hili kidunia ili lifahamike zaidi na zaidi.
 
Kusema kweli saiz kabila la kimasai halina maajabu tena ya kufanya tuwape kipaumbele kama kivutio cha watalii kwa kuwa maisha yao ni maisha ya kawaida kabisa, ukiachana na ufugaji wao na uvaaji wao hakuna kingine cha maajabu kinachofanya kutangazwa kama kivutio cha watalii,

Katika filamu ya Mama loyal tower yalifanyika makosa makubwa kama hawakukumbuka kuonesha Dunia maisha ya Wahadzabe,
Lugha zao tamaduni zao na ndoa zao, kusema ukweli Wahadzabe ni zaidi ya kivutio,

Saizi kumetokea wajanja walioijua fulsa na kuichangamkia wanapiga pesa kupitia kuonesha maisha ya kabila hili kupitia mitandao ya kijamii, kama youtube na sehem zingine, na watu wao ambao wamegundua fulsa hii saizi wamejizolea Umaarufu na wafuasi kibao na wafuatiliaje ndani na nje ya Inchi ambao wanafuatilia maisha ya hawa jamaa,
Huku taifa likiwa bado halijagungundua kuwa ipo haja ya kuwekeza nguvu kupromote Tamaduni za watu hawa na kufanya kama chanzo cha utalii wa wawatu kuja kujionea maisha ya Jamii hii ya watu wanaoshangaza.

Na yafuatayo ni miongoni mwa mambo ambayo yanashangaza katika kabila hili.

1. Aina yao ya uwindaji
2.Ndoa zao
3 .Vyakula vyao
4.Makazi yao,
5. Usafi wao
6. Mavazi yao
7.Mawasliano yao,
8. Ushirikiano wao.
9. Misiba yao.
10. Uongozi wao.

Jamii hii imekuwa iko tofauti kabisa na Maisha ya jamii zote tunazozifaham sisi ila cha ajabu wanaopewa promotion kama vivutio ni Maasai ambao kimsingi hawana maajabu yoyote zaidi ya kuzurula na mavibuyu mikononi na kulinda mageti.

Baada ya kutokea baadhi ya watu kustukia fulsa za kuonesha maisha ya hawa watu kupitia mitandao ya kijamii, Hatmae hii limewafikia Clouds Media na kuwapelekea kuomba mahojiano na vijana wa kabila hili kusema kwel mahojiano hayo yamekuwa na mvuto na watazamaji wengi sana baada ya kushtushwa na maisha ya watu wa jamii hii. Nataman kama leo tungetumia nguvu kutangaza Kabila hili kidunia ili lifahamike zaidi na zaidi.
Daah,
Uongo siyo mzuri, mi nilivutiwa kwenye ndoa basi, yaani nyani dume anatosha kuoa mke fresh bila chenga looh.
 
dunia ya leo haitaki watu sampuli ya wahazabe. ni hasara

wote walitakiwa watolewe maporini waanze shule
Ujue mbumbumbu wana furaha sana huku duniani. Jamaa zetu hawa wanajua kitu kimoja tu kuwa The Sun ni mumewe na The moon na Stars ni watoto wao basi. The sun akizama wanajua mumewe the Moon kachoka na sisi tukalale. Hizo habari zingine haziwahusu, the sun akiamka nao wanaamka kwenda kutafuta asali.
 
Mkuu kama hayo maisha wanayapenda na kuyafurahia na kamwe serkali haijawahi kuwalazimisha kwanini uwaone mbumbumbu ili hali hata sisi tunachokiabudu hatujawahi kukiona heri wao wanakiona daily?
 
Ya Wahadzabe, historia tosha na facts kuhusu mabadiliko ya binadamu, Homo sapiens.

Homo Evolution.

Hunter gethering!!

Kabla ya Inventions za Nation's, Money, God's/god's/Mono.
 
kwa jinsi wadau wa watalii walivyo makini kusaka fursa, nadhani;

1. wamewaona wahadzabe, lakini wahadzabe wenyewe wamekataa kufanyika kitega uchumi, kuguezwa 'cultural mascots' kama wamaasai

2. serikali inasita kujihusisha nao, ikiogopa milolongo ya sintofahamu kama ilivyo kwa wamaasai

au labda wadau pamoja na serikali hawako makini kiviiile, hawajashtuka tu
 
Back
Top Bottom