Wahalifu siyo wa kucheka nao, hiki ndicho walichofanya El Salvador

Kuna Ecuador pia nimeona wahalifu wamechafua nchi.
Wqhalifu wamechafua nchi
Na wahalifu wote huko wanaungana
Kupambana na serikali
Serikali ikitumia nguvu na wao wanatumia nguvu
Serikali ikae chini iangalie namna ya kupunguza uhalifu,uhalifu unapungua kutoka kwa hao hao wahalifu
Na ukiona nchi ni failed state basi kuna shida na watu wanaamua kutafuta utawala wao

Ova
 
Msiisahau Haiti. Ambao wameomba msaada wa polisi milioni toka umoja wa mataifa, na Kenya inapeleka laki moja ili kukabiliana na wahalifu.
Haiti huko makundi ya wahalifu ndy wana ongoza nchi
Polisi na majeshi ya Haiti wamesanda

Ova
 
Mkuu, wew kuwa civilized haimaanishi watu wote wapo civilized, sometimes mbinu pekee ya kudeal na wahalifu ni shaba tu, ukiwachekea nao watakuangushia mzigo,

Hio ni sababu hata USA wana magereza ya kikatili na wanatoa adhabu ya kifo, usicheke na kima kabisa
 
Uhalifu wa South Africa ni suala la kihistoria zaidi kuanzia kutoka utawala wa apartheid wa makaburu na mapambano yake. Silaha zilizotumika katika mapambano hayo na kushambuliana katika misingi ya rangi bado ziko nyingi na zimezagaa mitaani. Jambo lingine baadhi ya maeneo ya watu weusi huku Africa Kusini yana umaskini wa kutisha na hali mbaya sana ya upatikanaji wa huduma za kijamii. Haya ukichanganya na pengo kubwa sana la matajiri na masikini pamoja na ufisadi uliokithiri hali ya uhalifu lazima iwe mbaya sana.
 
Hawa jamaa wanakuja mchana kweupe kusafisha mchana kisa mbwa tu kapotea.
Tulioshudia haya wacha tukae kimya.
 
Ma shaa Allah

Sasa awapelekee Masheikh wawe wanawapiga daawa magerezani, kama wanavyofanya USA.
 
Kwa nini nchi za Ulaya na baadhi ya nchi kama Japan na Canada zina kiwango kidogo sana cha uhalifu??
 
Dawa ya uhalifu duniani ni kuwa na Sharia.
 
Ma shaa Allah

Sasa awapelekee Masheikh wawe wanawapiga daawa magerezani, kama wanavyofanya USA.
Nchi za Ulaya Magharibi na Scandinavian, Japan na Canada ndizo nchi zenye viwango vidogo sana vya uhalifu na hukuna masheikh wanaopiga daawa magerezani.
 
Dawa ya uhalifu duniani ni kuwa na Sharia.
Mbona Ulaya Magharibi, Scandinavian, Japan na Canada hakuna Sharia ila ndio nchi zenye viwango kidogo zaidi vya uhalifu duniani??
 
Mbona Ulaya Magharibi, Scandinavian, Japan na Canada hakuna Sharia ila ndio nchi zenye viwango kidogo zaidi vya uhalifu duniani??
Weka ushahidi wa sheria zao.
 
Vifo kutokana na mauaji kati ya watu 100,000 vilitoka 53 hadi 2.4! Leo watu wengi wanashangilia hilo. Bahati mbaya au nzuri vyombo vya haki za binadamu vimeanza kupiga kelele kuwa anashikilia watu kinyume na sheria!!
MAshirika ya haki za binadamu ni wapumbavu sana. Kwanini hawapigi makelele pale magenge ya wahalifu yanapofanya utekaji na mauaji? Kwao haki za wahalifu ni bora zaidi kuliko uhai wa raia unanyakuliwa na magenge hayo.
 
Haiti huko makundi ya wahalifu ndy wana ongoza nchi
Polisi na majeshi ya Haiti wamesanda

Ova
Haiti ni dola lilishondwa, sawa tu na Somalia, Yemen na Afghanistan. Wa-Ecuador waliposhika wasiachilie. Hapo hapo waendelee kukaza. Hakuna kuongea na wahalifu.
 
MAshirika ya haki za binadamu ni wapumbavu sana. Kwanini hawapigi makelele pale magenge ya wahalifu yanapofanya utekaji na mauaji? Kwao haki za wahalifu ni bora zaidi kuliko uhai wa raia unanyakuliwa na magenge hayo.
Kuna mhalifu akamlaumu mhalifu?
 
Weka ushahidi wa sheria zao.
Hakuna nchi ya Ulaya yenye Sharia, Japan na Canada hakuna Sharia pia.
Wewe ndiye unapaswa kuweka ushahidi wa kwamba hizo nchi zina Sharia.
"Huko shuleni ulienda kusomea ujinga ?"
 
Kwa nini nchi za Ulaya na baadhi ya nchi kama Japan na Canada zina kiwango kidogo sana cha uhalifu??
Kasome history ya Japan, Wajapan hawa wamestaarabika miaka ya karibuni, ila wamenyooshana sana huko nyuma, same to SK,

Kuhusu canada kuna jamii ndio zina ustaarabu damuni,
Ila kubali kataa, kuna level ya criminal activities ikifika dawa ni kurudishana kwa Mungu tu, same to panya road hapa bongo, sema hapa huwa hatufanyi intensive sana, ila kama unakumbuka walitaka kuja, wakawahishwa kadhaa kwa Mungu pakatulia, wamerudi tena wengine wamewahishwa, unaona kuna utulivu,

Watu wengine wanakuwa wameharibika beyond repair, hao unawapiga jela maisha au unawarudisha kwa Mungu,

Et leo umpeleke veta yule Dangote wa Chuga kisha umpe 4M ajiajiri unadhani ataacha uhalifu ?
 
Daah aisee hayo magenge ya madawa ya kulevya ni hatari sana huwa awajali kitu nadhani hiyo ni dawa moja nzuri hata SA wangefanya hivyo uhalifu ungepungua kabisa..jamaa wanasota aisee hakuna rangi wanaacha kuona siku wakiamua kuwahesabu...
 
Msiisahau Haiti. Ambao wameomba msaada wa polisi milioni toka umoja wa mataifa, na Kenya inapeleka laki moja ili kukabiliana na wahalifu.
Laki moja watabaki na kitu kweli huko kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…