Makahama ya Kimataifa ya Uholanzi(International Court of Justices-ICJ) katika maamuzi yake jana kwenye kesi ya Serbia v. Croatia imesema "that it was now up to the justice systems in both countries, but also elsewhere, to prosecute those responsible for crimes"
Maamuzi hayo ni muafaka na ni onyo kwa Viongozi wetu wa Kiafrika ambao hupenda kung'ang'ania madaraka kwa kubadili Katiba na mwisho wanapokataliwa huleta vurugu inayopelekea maaji ya haraiki kama ilivyotokea RWANDA.
Nawasilisha kwa michango na mapendekezo
HAKUNA MAHAKAMA INAYOITWA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHOLANZI.
Uholanzi kuna mahakam tatu za kimataifa.
1. international court of justice (ICJ)...hii ni mahakama inayoshughulikia migogoro kati ya nchi na nchi, sio watu. mfano: malawi vs tz, serbia vs croatia etc.
2. International Criminal Tribunal for the Former Yugoslavia (ICTY). hii inashughulikia makosa ya uhalifu yaliyofanyika yugoslavia ya zamani kabla haijaparanganyika.
3. special Tribunal for Lebanon (STL). HII pia ipo the Hague Uholanzi. inashughulikia makosa ya uhalifu yaliyofanyika wakati wa vita vya wenyewe vilivyosababisha Rafik hariri kuuawa na wengine.
4. Special Tribunal for Siera Leone (STSL). hii pia ipo the Hague Uholanzi. inashughulikia makosa yaliyofanyika Sierra Leone.
2. International Criminal Court( ICC). hii sio mahakama ya kivita kama wengi mnavyoitaja, hii ni mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai. hii inashughulikia binadamu, haishughulikii nchi (states). mfano, mtu yeyote akifanya kosa linalodondokea sheria ya mahakama hii inayoitwa ICC STATUTE au waweza kuita ROME STATUTE OF INTERNATIONAL CRIMINAL COURT, anashitakiwa pale. arrest warrant itatolewa na nchi wanachama watakamata mtuhumiwa. mahakama hii imekuja kuwa mbadala ya mahakama za muda (ad hoc tribunals )kama Rwanda ICTR n.k.
ad hoc tribunals ni kama STSL, STL, ICTR NA ICTY. yaani mahakama za muda tu, zina limit muda ukifika zinakoma kufanya kazi na makosa yake yamelengwa makosa ya muda fulani tu. ICC imekuja baadaye ili kufuta hizi limit, makosa yote yaliyofanyika tangu July moja 2002 na kuendelea milele, mtu atapelekwa ICC na si mahakama zingine. hiyo imewekwa kuwa mahakama ya kimataifa ya kudumu itakayoshitaki watu/individuals na siso states kama ulivyo sema wewe (umesema serbia vs croatia).
however, nimefurahi umeleta topic, hii ni topic nzuri na watu wanatakiwa kufahamu kuwa wakifanya chochote wanaweza kufikishwa ICC. however, ukiwa unaongelea suala hili, jua kuwa ICC sio mahakama ya kivita, ni mahakama ya makosa ya jinai ya kimataifa ambayo ni machache tu yamechaguliwa Genocide, crime against humanity, war crimes and crime of aggression.