Nani kakudanganya kwamba zoezi la kuwaondosha wahamiaji haramu linahusu wanyarwanda peke yao?,pia tumia muda kidogo kujifunza kuhusu masuala ya uraia.Inaonyesha uelewa wako ni mdogo sana kuhusu citizenship na jinsi uraia wa nchi unavyopatikana na aina zake.Suala la kabila la mtu linaweza lisiwe na uhusiano na uraia wake mfano kuna wasukuma,wagogo na wazaramo ambao si raia wa TZ baada ya kuukana uraia wa Tanzania,wakirejea nchini na kuishi bila kufuata utaratibu wanakuwa wahamiaji haramu.Mfano mwingine ni kwamba kuna watu walikuwa raia wa nchi nyingine lakini baada ya kuishi TZ kwa kipindi fulani na kutimiza masharti mengine muhimu waliamua kuomba uraia wa TZ,moja ya masharti ni kuukana uraia wa nchi zao kwani hapa TZ hakuna uraia wa nchi mbili,hata hivyo watu hawa hawayakani makabila yao wanabaki kuwa wahutu,watusi,waasia,nk raia wa TZ.