Wahandisi tunataka kila anayejenga ghorofa lazima usanifu na ujenzi atumie wahandisi

Wahandisi tunataka kila anayejenga ghorofa lazima usanifu na ujenzi atumie wahandisi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Kama kufungua biashara ya duka la dawa ni lazima udhaminiwe na dakitari inakuwaje shughuli za kihandisi zinafanyika bila kuhusisha wahandisi.

Kufungua gereji, ujenzi wa majengo ya gharama, sehemu za kuchomelea, n.k yote haya yanafanyika holela.

Kama madaktari wameweza hivi sisi wahandisi tunashindwa nini?

Nadhani tofauti kubwa ni madaktari wanacho chama strong kinachowatetea na sisi wahandisi tupo tupo tu.

Ni lazima jamii ijenge mazingira ya kujiri wataalamu inaowasomesha.
 
Wazo zuri na moja ya njia ya kuwaajiri wahandisi na thamani yao itonekana na kazi zao zitapatikana kwa wingi na ujanja ujanja utaepukika pia majengo yaliyochini ya viwango na yenye kuleta hatari ya kudondoka yata sahaulika na kudhibiwa haawaa..
 
Kwa nini msianzie na nyumba za kawaida? Kila jengo linahitaji usanifu, hapo ndio mnapofeli mnapoanza kubagua majengo. Wenzenu madaktati kila anayedili na mtu lazima awe amequalify na amepitishwa. nyie mnachagua baadhi ya majengo halafu bei zenu sio rafiki kwa watanzania
 
Sisi kama wahandisi tungefurahi kuona jamii inatutumia katika kufanya shughuli za kihandisi katika jamii.

Unajua yapo mambo ambayo jamii inayafanya kwa kutojua na kuingiza jamii katika gharama zisizo za msingi na tungependa kuona jamii inapata majibu ya kitaalamu ambayo yatatengeneza ajira kwa wataalamu wetu na kuisaidia jamii kuepuka gharama zisizo za lazima au kuongeza thamani katika makazi yao
 
Sisi kama wahandisi tungefurahi kuona jamii inatutumia katika kufanya shughuli za kihandisi katika jamii.

unajua yapo mambo ambayo jamii inayafanya kwa kutojua na kuingiza jamii katika gharama zisizo za msingi na tungependa kuona jamii inapata majibu ya kitaalamu ambayo yatatengeneza ajira kwa wataalamu wetu na kuisaidia jamii kuepuka gharama zisizo za lazima au kuongeza thamani katika makazi yao
Fani yenu sio rafiki kwa jamii ya watu wenye kipato cha chini hata kidogo. Na pia kuna alternative kwenye kazi yenu, kwa kuwa kuna mafundi mitaani wanafanya kazi zenu kwa ufanisi mkubwa sana na hamna risk yoyote kuwatumia tofauti na madaktari one mistake one goal.
 
Siku ghorofa lako likikuangukia ndio utajua umuhimu wa wahandisi.
 
Mnatishia nyau. Umeona lini ghorofa limeanguka Bongo? Mpaka maghorofa ya udongo yanadunda tu.

Nyumba nachora mwenyewe natafuta local fundi wanajenga design za finishing nabuni mwenyewe na wapangaji napata
Ukienda mtaani unakuta mtu anajenga nyumba ya kigorofa kimoja, chini anasimamisha nguzo za zege alafu analaza tofali zote za ile sehemu ya chini. huku ni kuongeza gharama za ujenzi ambako kama wangekuwa wanatumia wataalamu bila shaka gharama zingepungua.

Unakuta mtu anajenga nyumba kwa kujitahidi kuweka choo cha public na masta ya nyumba karibu ili etu kupunguza gharama. gharama anazopunguza ni bomba za maji machafu ambazo gharama yake ni ndogo sana na akienda kuezeka anaezeka kama kanisa.

Jamii inatumia umbumbumbu katika ujenzi ambao wataalamu wakitumika gharama za ujenzi zitapungua na ubora utaongezeka
 
Kama kufungua biashara ya duka la dawa ni lazima udhaminiwe na dakitari inakuwaje shughuli za kihandisi zinafanyika bila kuhusisha wahandisi.

Kufungua gereji, ujenzi wa majengo ya gharama, sehemu za kuchomelea, n.k yote haya yanafanyika holela.

Kama madaktari wameweza hivi sisi wahandisi tunashindwa nini?

Nadhani tofauti kubwa ni madaktari wanacho chama strong kinachowatetea na sisi wahandisi tupo tupo tu.

Ni lazima jamii ijenge mazingira ya kujiri wataalamu inaowasomesha.
Tatizo kwanza waandisi watanzania ni vihiyo hata aliyewafundisha hawaamini, jipangeni kiweledi kwanza muweze kushinda kandarasi kubwa zinazochukuliwa na wageni hapa nchini ndiyo mje na upumbavu wenu
 
tatizo kwanza waandisi watanzania ni vihiyo hata aliyewafundisha hawaamini, jipangeni kiweledi kwanza muweze kushinda kandarasi kubwa zinazochukuliwa na wageni hapa nchini ndiyo mje na upumbavu wenu
Hii tunaita kuendesha nchi kwa kutumia umbumbumbu.

Shule peke yake haimfanyi mtu kubobea katika fani yake bali shule pamoja na exposure baada ya shule.

unachokisema ni african mentality ambayo imeendelea kutafuna jamii zenu. mfano unakuta waafrika wakipata mali basi hawawashirikishi watoto wao waone na kujifunza jinsi baba yao alivyotafuta utajiri bali huamini watoto wahangaike kivyao kutafuta yao. Matokeo ya haya ni baba kuondoka alikuwa na mali lakini akifa ndiyo watoto wanapata fursa ya kuingia kwenye kile alichokuwa akimiriki baba yao na kwa kukosa maarifa huanza kugombania mali na kuzipora.

haya ndiyo tunafanya katika kuongoza nchi zetu. tunauza rasilimali za taifa kama madini, mazao ya kilimo na kadhalika na badala ya kuwapa watoto wetu nafasi, tunawatenga na kuwapa wageni. matokeo yake ni watoto hawa kuwaza kuiba tu maana hawajui mbinu za kutafuta.

nichukulie mfano wa china, asilimia 90 ya makampuni ya kichina yanayofanya kazi huku kwetu yanamirikiwa na serikali ya china na yanatumia wafungwa kufanya kazi. bado wachina, wahindi wakikukopesha pesa wanajitahidi utumie wakandarasi wao na kununua bidhaa za mradi kutoka kwao.

Hizi ni mbinu za kiuchumi kutengeneza ajira kwa watu wao na kutaka kuuza bidhaa zao.

hata sisi tunatakiwa kuiga tu na kuanza kutengeneza ajira kwa watu wao.
 
Hii tunaita kuendesha nchi kwa kutumia umbumbumbu.

Shule peke yake haimfanyi mtu kubobea katika fani yake bali shule pamoja na exposure baada ya shule.

unachokisema ni african mentality ambayo imeendelea kutafuna jamii zenu. mfano unakuta
Umeme a kweli mkuu
 
ukienda mtaani unakuta mtu anajenga nyumba ya kigorofa kimoja, chini anasimamisha nguzo za zege alafu analaza tofali zote za ile sehemu ya chini. huku ni kuongeza gharama za ujenzi ambako kama wangekuwa wanatumia wataalamu bila shaka gharama zingepungua.

unakuta mtu anajenga nyumba kwa kujitahidi kuweka choo cha public na masta ya nyumba
Mie nimejenga ghorofa moja na nimetumia Architecture kuchora, QS kufanya makadirio na Engineer amesimamia lakini tofali za chini wamelaza na nguzo zimewekwa unataka kusema wote hao ni mbumbumbu?
 
Na sisi wanauchumi wazalendo tunataka kila tofali, nondo,kokoto ,bati ama vigae vitakavyotumika viwekewe tozo
IMG_20210717_151323.jpg
 
Mnatishia nyau. Umeona lini ghorofa limeanguka Bongo? Mpaka maghorofa ya udongo yanadunda tu.

Nyumba nachora mwenyewe natafuta local fundi wanajenga design za finishing nabuni mwenyewe na wapangaji napata
Kuna sababu kwanini watu wanasomea majengo miaka minne na wengine mitano chuoni.
 
Mie nimejenga ghorofa moja na nimetumia Architecture kuchora, QS kufanya makadirio na Engineer amesimamia lakini tofali za chini wamelaza na nguzo zimewekwa unataka kusema wote hao ni mbumbumbu?
Hata mafundi wa kawaida wanajiita ma engineer na ndiyo hao umekutana nao
 
Back
Top Bottom