Morani,
Najaribu kufahamu vitu gani tunatengeneza Tanzania, maana najua vitu kama machinery sisi ni wanunuzi.
Asante sana kwa input yako. Nina interest ya end-product ili nitengeneze common ground halafu nilete teknolojia mpya itakayo fanya u-improve end-product yako. So hapa naangalia 3D products.
Kitu relevant sana hapo ulichosema ni Architecture. Hiyo 3DstudioMax ninayo ofisini ila sijapata muda kuitumia maana inatoa 3D tu image tour na haisadii real issues.
Kwenye Architecture, end product ni nyumba. Interest hapa inakuwa kama kuangalia ventilation system na labda forces/stresses katika kuta/misingi za majengo etc kabla hata hujaanza kujenga hiyo nyumba (Vitu hivi vingi ma-Architects na Engineers wanapiga mahesabu kwa mkono au wanafanya maamuzi through experience......ndio mambo ya majengo kuanguka huko China). Wajenzi wenye pesa kubwa wanaweza ku-justify hii teknolojia. Pia katika njia hii, kwamfano benki za Tanzania zinaanza kutumia tecknolojia mpya, makompyuta/servers kibao etc Je, wanajenga data centres zao vipi? Na ku-maintain vipi?
Kitu kingine, ni mfano wa 'mouldings' kama za maplastiki etc. Moulding ni final product. Basi ningependa kujua hizo final products ni nini na zimetengenezwa vipi.
Kuhusu vitu kama barabara, safi, lakini hapa naona interest zaidi itakuwa ni machine yenyewe inavyofanya kazi, kwa mfano machine ya kuchanganya zege au hata kukandamiza rami etc. Machinery inaweza kuwa hata hiyo ya 'Moulding', au mashine ya kupepeta mchanga kwenye madini. Lakini hatutengenezi machinery as such Tanzania, tunanunua. Lakini nikijua machine tulizonazo zinatengeneza nini na nikaelewa teknolojia inayotumika, pia naweza shauri nini kifanyike ili upate product nzuri zaidi and if possible cheaply. Main point here is, increasing efficiency of cost of production and better product.
Sijui unanipata? Nina haraka kidogo, nitarudi nisawazishe kama siko clear. Ila ishu ni kwamba nataka kujua mahitaji ya Tanzania. Teknolojia ni ghali, ila nina-negotiate njia ya kuifanya iwe accessible na bei nzuri zaidi kwa Tanzania, nikiwa kama consultant katika muda wangu. The fact natoka Tanzania, nimeweza ku-justify kwamba ni muhimu nichangie nchi ninayotoka huku nikipima affordability. Nikielewa mahitaji, inakuwa rahisi kujustify.