Kwa uzoefu wangu mdogo, tofali zenye uwazi katikati (Hollow Cement Block) zinatumika kwa uchache sana. Pamoja na faida zake nyingi, najiuliza ni kwa nini?
Sababu kwanini hayatumiki sana
1.Hayana uwezo wa kubeba mzigo mkubwa (Non load bearing wall).
2.Malighafi za kuyatengeneza hazipatikani kwa urahisi (hasa chipping /clusher dust).
3.Kuta nyingi za maofisini kutumia Aluminium (uwezo wa kuweka na kuondoa).
4.Kama hazitojazwa ndani yake kwa malighafi maalum (insulator /pumba za mbao n.k) huleta joto ndani ya nyumba /cracks).
5.Haziwezi kutumika tena.
6.Hasara katika usafirishaji hasa pale zinapokuwa hazina viwango.
7.Matumizi yake yanahitaji uangalifu hasa kuyakata /joints hivyo kulazimisha vifaa maalum kuyakata ili vipande vungine vitumike kwenye ujenzi.
8.Ni rahisi kutoboa na kuingia ndani /kiusalama si sawa hasa kama jengo ni la chini.
9.Bei kuwa kubwa pengine kuzidi yaliyo na ujazo ndani.
10.Hupatikanaji wake kuwa mgumu.
11.Wajenzi na wenye Ujenzi kutokuyaamini ingawa ni mazuri kama watajitokeza kufuata Ushauri wa kitaalamu kwa Wataalamu wa Majenzi (Kujenga ki Mazoea).
12.Kupunguza uimara wa ukuta hasa unapojenga jengo lenye kima kirefu (Maghala, Makanisa, Karakana n.k) bila kuweka nguzo na mikanda ya zege /beams hivyo kusababisha jengo kuezuliwa au kupata ya nyufa za kulizunguka jengo.
Faida za haya matofari zipo nyingi kuliko hasara ambazo ni
1.......40.
Ili kupata faida hizo tembelea Wataalamu wa Ujenzi popote ulipo.