Wahanga hawa wako wengi-Mama, mtoto wafia mapokezi ya hospitali kwa kukataliwa huduma

swala ni kudeal na mamlaka zinazohusika ili kuliondoa hili tatizo..

The most effective of dealing with this in this age of market system is through the market, by not enrolling into nursing.

A shortage of nurses will come about and they will realize how important nurses are, they will raise wages and working conditions.

My thing is you cannot sign up knowing how deplorable conditions are and then embark on a strike that will jeopardize peoples life, after you signed up nonetheless.

I understand the problem is with the biggerheads, lakini sisi wenyewe kama wananchi (hao wanaokubali kuwa nurses bila ya kuangalia maslahi kwanza kabla ya ku sign up) tunaendekeza sana njaa na matatizo yake ndiyo haya.Watu wanataka kuajiriwa tu bila kuangalia maslahi, wakiajiriwa ndiyo wanalalamika maslahi madogo, conditions mbaya.Uswahili mtupu!

Kwangu mimi ukishakuwa nurse maana yake umechukua risk ya kufa, that is bigger than any money/ resources issue.Sasa kwa nini uchukue risk ya kufa wakati wewe uko concerned sana na mshiko kuliko hata maisha yangu?

Au ni geresha tu ili mradi upate ajira?

Kuna story moja ya Engineer aliyekuwa analalamika kuwa engineers hawapati ujiko bali kila kitu kizuri kikijengwa anayepata ujiko ni architect, engineer mwingine akamjibu akamwambia kama unataka ujiko nenda Hollywood kawe actor.

Kuna kazi nyingine zinataka moyo wa sacrifice na tusitake kuwatetea wauaji eti kwa sababu ya conditions na mishahara.I understand they gotta eat and all, but damn, do they have to kill somebody? Kama wao kinachowa motivate ni mishahara they are in the wrong profession.
 
Hao wafanyakazi hawana tofauti na viongozi wa ccm wanaonunua ndege na rada mbovu kwa bei za kuruka na kuuza nchi kwa bei za karanga huku wakiacha watz wakila nyasi (kama alivyosema Mramba).

Jamani yaani inatia huruma na hasira ... yaani acha tu.

pumba ! manesi na viongozi wa ccm wapi na wapi ? pumba tupu zinakutoka !
 

i wish wengi humu wangekuwa na mind kama yako !
 
Alitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na 'glovu' (mipira ya kuvaa mikononi), pamba, sindano, dawa za maumivu na maji ya uchungu.

Kama serekali inadai kuwa huduma kwa wajawazito ni bure, sioni kwanini hivyo vitu hapo juu visiwe bure. Hawa wauguzi waliohusika na tukio hili siwezi kuwashambulia directly kwa kuwa nahisi wali act according to policies zilizowekwa na 'wakubwa'.Ninachojua ni kwamba mjazito anatakiwa atoe shilingi elfu tano akienda kujifungua na serekali ina assume kwamba kila mtu atakuwa nayo.
 

Kwani hawa unaowatetea wamelazimishwa kufanya hizo kazi? Kwa mshahara huo? Kama mambo ni pesa kwa nini hao ma surgeon wasiende kupiga deki TRL? Tusiendekeze uzembe kwa kusingizia malipo duni. Wameamua kufanya hiyo kazi basi waifanye kwa uadilifu. Wakiona hawawezi, wawapishe wenzao wao wawafuate wenzao ughaibuni au kwenye siasa. Hao ma surgeon unaowatetea wamebanana kwenye mahospitali binafsi ambako wanafanya wanachokiita konsaltansi. Hawataki kuondoka Muhimbili na hospitali za serikali kwa sababu wanazitumia kama back up(maabara, support staff n.k.) ya konsaltansiz zao. Nesi anayemwangalia mja mzito anakufa kwa sababu hana glavu hastahili kubaki kwenye ajira. Uongozi unaoruhusu mwananchi wake afe kwa sababu ya kukosa glavu haustahili kuongoza.

Amandla!
 

Duh!!! Maskini ya mungu! Mwenyezi azipumzishe roho zao mahali pema peponi. Ndugu na jamaa wa marehemu wawafungulie mashtaka hospitali ya Mwananyamala kwa uzembe uliosababisha kifo cha mama na mtoto ili walipwe fidia.
 
Usalama wa taifa mpo hapo??? Nina uhakika ikiwa Usalama wa Taifa watafuatilia hilo wataona mengi. Nendeni Amana, Temeke, na hata Muhimbili kote huko ni hayo hayo.
 

mzee Pundit.. viapo vingekuwa vinamaana Tanzania unajua tusingefika huku tulikofika. Nadhani kwa wengi viapo ni kama alama ya box tu ambapo unatakiwa utiki yaishe..
 
tupitishe petition Mwakyusa must Go maana sijui anafanya nini pale... madaktari wanaacha kutibu wanakimbilia researches na kutimkia nje je kweli hii serikali inajali maisha ya watu wake kweli??
nina hasira siyo kidogo

serikali yooote kimyaaaa nw iko busy na sullivan sijui nin,
may their souls rest in peace...
ndio maana jana nikauliza hivi bongo ya sasa ni sekta gani iko na amaniii??
hivi ingekua huyo mama anaishiwa na jina la ukoo kama kikwete,lowasa etc etc hii kesi ingenyamaziwa??
may b lets wait kwa vile ni mlalahoi mwenzetu serikali ikimalizana na kina chris tucker kule arusha utasikia waziri husika anakwambia tunaunda tume kuchunguza....in which ni pesa zetu tena zatumika n de report wil b kutupwad kapuni as usual!!!yan ndo itakua kimoja hivyooo
inauma sana...nikifikiria,huwaga mi nalia............................
 
''Marehemu aliletwa hapa wodini akiwa na hali mbaya na ninadhani alishafariki kwani alipoletwa akalazwa kitandani kisha akazungushiwa pazia la kijani na ndani ya pazia hilo kulikuwa na wauguzi watatu huku mmoja akiingia na kutoka. Na baada ya hapo hawakuelewa kilichoendelea,'' alisema na kuongeza:

Sitetei uoza lakini ukiangalia statement hizo juu utaona kuwa mama huyo alifika akiwa moribund patient, na alizungukwa na manesi ambao walikuwa wakiingia na kutoka (walikua wanahangaikia kitu fulani?) je hapo mtasema hakushughulikiwa? yaonekana wazi huyo mgonjwa alifika mahututi ingawa vital sign zake( BP.Pulse rate, Record ya uchungu-Partogram etc) hatuzijui hivyo kulaumu moja kwa moja kuwa kuna uzembe mara ccm nakadhalika bila ushahidi wa kitaalamu inakuwa ngumu kidogo.na pia jamani kufiwa nako inauma hivyo ni rahisi kumtupia lawama mtu mwingine ukasahau ya kwako. ni vipi ukiambiwa kuwa alicheleweshwa akiwa kwa mganga wa kienyeji na alifika hapo beyond repair? ni vipi ukiambiwa kuwa alikuwa kapewa KOMBE na likam- intoxicate???ikumbukwe kuwa katika mahospitali yetu mtu akifa huachwa kidogo mpaka apoe (sijui nani alitunga hiyo) ndipo hupelekwa Mortuary sasa yaweza kuwa ndivyo sivyo na akina Lunyungu wakadai katelekezwa
 
Sina cha kusema inasikitisha sana na matukio haya sio mara moja.Yapo yale ambayo yanatokea wahanga wanazibwa midomo wasitoe siri hadharani kwa ajili ya kibarua cha fulani. Na yapo mengine ambayo watu hutishiwa na haya machache tunayoyasikia na kwa sababu ya uerevu wa watu tu . Yale ya kichwa na miguu ya MOI nadhani bado yanakereketa masikioni mwetu.Kuna wakati mwingine watu wanafanya kazi na kutotilia umuhimu wa kazi yao hususan linapokuja suala la maslahi. Ubinafsi,professionalism,nepotism vinatuunguza kidogokidogo.
 
Kufanya research ni sawa kabisa, ila tatizo ni serikali, maana inawezekana hizo research zinafanyika nchi za watu na kuwanufaisha wengine wakati watanzania wakiendelea kufa tu

Inauma sana.

Mkuu hawa wanaofanya research huko ni katika kutafuta mahala ambapo wanathaminiwa. Sisi serikali zetu zimekalia siasa siasa tu hakuna cha kuwaangalia wataalamu, asikudanganye mtu uwezi ukaadhirika wakati una utaalamu wako na unatakiwa mahala pengine. Huwa wanasema wema usizidi uwezo.
 


Kinte
Naomba sema tena habati hii kwa makini .Kuna 2 stories in one .Habari ya kuzungushiwa pazia imesemwa na Mama aliyeko wodini juu ya mtu mwingine aliyekufa kabla ya huyu tunaye mlalamikia hapa .Lakini mimi nawapa onyo Mungu hamfichi mnafiki kuna siku yatawafika makubwa ya aina hii kwa uzembe sijui kama mtakuja hapa na kusema haya .

Soma umetulia utaona habaro 2 ndani ya hii moja .Usikurupuke .
 
Kwa uzembe Mwananyamala Hospital ni wazembe kupindukia kuna Gynecology mmoja yupo pale ana case za uzembe kibao alihamishwa kutoka Amana Hosp kwa ajili hiyo hiyo huyo mama atakuwa amekufa kwa uzembe, inasikitisha sana pole yao waliopoteza mama na mwana.
 
habari hizi zimenitia huzuni sana ... bora nisingesoma.

Wameshatukuta na sisi

Mzazi kazidiwa tukapewa rufaa muhimbili ... mgonjwa akawa anatizamwa kama nyani kwenye cage ... tulivyoona mda unazidi kwenda na kitoto tumboni kinazidi kupigania uhai .. tukawaambia kwamba Amana tuliambiwa kwamba mtoto anaishiwa nguvu afanyiwe upasuwaji haraka mzazi ... walitujibu kwamba amana ni kichanga kwao kwani muhimbili ndiyo mama kama si bibi wao.. tukajaribu kuhonga wee .. ubaya hatukujuwa nani alikuwa kwenye zamu maana wote walochukuwa hongo waliondoka huku zamu wakiwaachia wengine wapya.

To cut the long story short , siku ya pili tena usiku mzazi kapasuliwa ... kitoto tukakikosa ...

Laana ya Mungu iwafikiye maana wanawauwa mama na dada zetu na malaika wa Mungu wasiokuwa na hatia
 



hiyo argument yako kwa tanzania bado sana.Wanafunzi wengi wa kitanzania wako vyuoni lakini hawajui focus yao ni nini.Wanachukuliwa wanapelekwa kusomea unesi lakini hakuna mwenye utafiti tayari wa kujua mazingira ya unesi yakoje na nesi wa tanzania analipwa nini.
Kifupi mwanafunzi ana enroll kozi ama kwa kufuata mkumbo ama kwa vile taasisi ile imekuja kumchagua tu afanye ile kozi.
Kwahiyo mimi sioni mantiki ya kusema eti walaumie kwa vile wamekwenda wenyewe kufanya hospitali.
Hivi wewe unafikiri hizi hospitali zetu tayari zina manesi wa kutosha?
Kama tunataka maendeleo ya kweli basi ni lazima tukubali kuheshimu professions za watu,tukubali kuwa kwa kufanya kazi yoyote(si unesi,udaktari tu)yakupasa kuchukua risk kwa lolote ambalo litapelekea kuleta maslahi kwa jamii kubwa ya watu.Tuache kuwa wabinafsi na wanafiki.
 
kilichobaki wajimini mkiwa mwaenda hospitali kama hizo hata ka jina lako ni mwaimuna kikaragosi,badilisha jina jiite mwaimuna kikwete,raheli lowasa,fatuma shein,rose tibaigana,asha mwema..hata ukipenda ngozi nyeusi we jiite tu mwantumu rostam aziz...wakiona majina kama hayo huwa kusema kweli wanajitahidi mnoo otherwise waoneshe hela!
its a shame as if na wao siku moja hawatakuja zaa au pata shida yeyote wanasahau mganga hajigangi hata siku moja!
 

mkuu usiwe mvivu wa kusoma hebu jifarague na hii au rudi mwanzo wa thread kisha upost tena maana inaonesha hautetei uozo bali unaushabikia...


jitahidi mkuu
 
Haya matukio yote yanatufikisha mahali pamoja tu. "Tulipoangukia, na si tulipojikwaa". Mfumo mzima wa malezi katika familia na jamii kwa jumla hauwatayarishi wengi kubeba majukumu kwa umakini na uadilifu.

Elimu itolewayo na matarajio tunayojiandalia hayakidhi. Elimu iko duni, lakini pia mazingira ya kazi yako duni vilevile. Ni hii Vicious circle ndio inatuacha tuzunguke hapa hapa kila siku. Na ikitokea jambo ndipo tunakumbuka. Kuonyesha hii ndio hali halisi, jaribu kukumbuka matukio ya namna hii yametokea mara ngapi na nini kimefanywa kuonyesha kwamba halistahili, halitarudia na hata ikibidi kuchukua tahadhari kabla ya tukio. Kumbukumbu zangu zinanionyesha ni tunasahau kwa urahisi na watu hawajawajibishwa ipasavyo huenda ndio maana mambo haya yanarudia.

Pamoja na kuwa ni jukumu la serikali lakini kama wananchi haya ni matukio ya kila siku katika nyanja mbalimbali. Ni mpaka pale tutakapoamua kubadili mtazamo wetu kama watu binafsi, jamii ndipo tutaweza kuishinda hii hali. Mahali tulipofikia ni pabaya kweli. Kinachoonekana kwa sana na urahisi ni kunyoosha vidole nani kakosea na kakosea wapi.

Kama kianzio sio vibaya ila tukubali ni safari ndefu na ngumu. Maadili ni muhimu. Utu ni muhimu. Elimu bora ni muhimu. Lakini ajira nzuri pia muhimu. Mazingira mazuri ya kazi pia muhimu.

Sijui Mzee wa Vijisenti anajisikia vipi kwenye hali kama hii. Hizi ni zile priorities ambazo kama sio ubinafsi au malezi mabaya ya ulafi huko tulikolelewa au tulivyojilea, ndizo zingezingatiwa.

Masheikh, Mapadre, Wachungaji, Wazazi na jamii kwa ujumla tieni shime maadili yarudi. Ubinafsi, ukatili na uzembe umezidi.

Poleni waliofikwa na shida hii.
 
Jamani bonge la aibu aibu aibu sana sana tu mama mjamzito anakataliwa kujifungua kisa vifaa hospital kubwa kama Mwananyamala mmh aibu ufisadi hadi mahospital duh!! Mwakyusa tunaomba ajiuzuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…