Wahanga wa Kishindo ndani ya Simba

Wahanga wa Kishindo ndani ya Simba

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
Ama kwa hakika Maisha yanaenda kasi sana. Wachezaji waliokuwa magarasa kiasi cha kuwachukiza Wanasimba na kufikia hatua ya kutaka kutolewa kwa Mkopo Nyota zao zimeanza kung'aa masaa 72 tu baada ya mgomvi wao kuondoka.

Haitashangaza Miraji Athumani akiiibuka Mfungaji bora wa Mashindano ya Mapinduzi. Na yule Kiungo Kijiko Virasta Kahata mechi ya Jana dhidi ya Mtibwa ndiye kachaguliwa Man of The Match! Kagere ndiye kapewa kitambaa cha Unahodha kabisaaaa!

Wakati mwingine tuepuke kukata tamaa pale tunapohisi Maboss wetu wanatuwekea Mtima nyongo. Poleni sana Kahata, Sheva, Kagere Et Al kwa magumu yote mliyopitia chini ya Kishingo. Sisi wanaSimba Tunaimani na nyinyi endeleeni kuipambania timu mpaka tufike Nusu fainali ya Champions💪💪💪
 
Ama kwa hakika Maisha yanaenda kasi sana. Wachezaji waliokuwa magarasa kiasi cha kuwachukiza Wanasimba na kufikia hatua ya kutaka kutolewa kwa Mkopo Nyota zao zimeanza kung'aa masaa 72 tu baada ya mgomvi wao kuondoka...
Simba ipi?

Ndio timu gani?

Hatuifahamu,fafanua kidogo.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Labda ungesema ni nani aliyekuwa anapendelewa.

Hao wote kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipewa nafasi.

Ila kwa sababu wewe ni mtu wa majungu na kuhisi unaonewa kila sehemu basi unahamishia hisia zako kwa wwngine.

Pambana kila upatapo fursa na hata pale unapokuwa ukiitafuta.
 
Simba kuna wakati wanapoteza umakini kwenye usajiri.

Wachezaji wengi wa kimataifa wa Simba wana kiwango cha kawaida kabisa.

Kiwango ambacho kinazidiwa hata na wachezaji wa ndani wa timu ndogo ndogo kama Mtibwa, Yanga, Kagera Sugar nk.
 
Simba kuna wakati wanapoteza umakini kwenye usajiri.
Wachezaji wengi wa kimataifa wa Simba wana kiwango cha kawaida kabisa.
Kiwango ambacho kinazidiwa hata na wachezaji wa ndani wa timu ndogo ndogo kama Mtibwa, Yanga, Kagera Sugar nk.
Mkuuu, Yanga ni timu ndogo ndogo kweli Mkuu? Wanaoonekana wana Viwango huko timu ndogo ndogo kama akina Gadiel, Ajibu, Morrison, Duchu, Lamine Moro nk nk wamesajiliwa Simba lkn wote wanasugua Benchi tu.

Mchambuzi mmoja aliwahi kusema kwa sasa Mchezaji wa Yanga anayeweza kupenya kwenye Kikosi cha kwanza cha Simba ni Mukoko na Ntibazokiza tuuu, wengine wote ni magarasa!
 
Back
Top Bottom