Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
Dar es Salaam. Baadhi ya wahariri wanaounda Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wamehoji mpango wa Serikali kuendelea kugharamia miradi waliyodai haina tija kwa kuongeza kodi na tozo kwenye bajeti ya Serikali.
Wakizungumza leo Jumamosi Juni 19, 2021 katika mjadala wa uchambuzi wa bajeti ya Serikali ulioongozwa na makamu mwenyekiti wa TEF, Bakari Machumu, wahariri hao wametaja ujenzi wa daraja la Tanzanite na uwanja wa ndege wa Geita-Chato wakisema haina tija kwa Taifa.
“Kuna miradi haina tija, kwa mfano daraja la Tanzanite. Wakati linajengwa walisema ni kwa ajili ya kupunguza msongamano kwa jiji la Dar es Salaam, lakini tukiangalia watu wengi wa Masaki wameshahamia Dodoma, labda kama tunataka kulitumia kupigia picha za harusi,” amesema Joseph Kulangwa ambaye ni mhariri wa gazeti la Raia Mwema.
“Kuna uwanja wa ndege wa Geita, nikashindwa kuelewa kuwa ni wa Geita au ni wa Chato? Wanasema umekamilika kwa asilimia 95 na unahitaji fedha zaidi kuukamilisha, sasa najiuliza tija ya huu uwanja ni nini?”
Maoni hayo yameungwa mkono na Abdallah Majura akisema daraja la Tanzanite lingejengwa eneo la Dumila mkoani Morogoro ambako hujaa mafuriko wakati wa mvua.
“Nilitegemea daraja kama lile la Dumila ambapo hutokea foleni kubwa wakati wa mafuriko tunakwenda kuzungukia Kilosa. Sasa unakuja kuwakamua wananchi kwa ajili ya daraja la Tanzanite ambalo nikiangalia Masaki hakuna foleni kubwa kiasi hicho,” amesema.
Majura amegusia mafuriko katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam akisema manufaa ya fedha za wananchi yangeonekana.
“Ni mara 100 wangejenga lile daraja la juu kutoka Magomeni Mapipa mpaka Fire. Kwa hiyo Mtanzania akikamuliwa ajue ni kwa ajili ya maendeleo,” amesema Majura.
Kwa upande wake Imma Mbuguni ambaye ni mhariri wa Majira amesema bajeti hiyo haijaeleza jinsi itakavyoikwamua sekta binafsi ili kuongeza uzalishaji na kukuza kipato.
“Ili Serikali ikusanye mapato inabidi sekta binafsi iwe vizuri. Ukiangalia sekta binafsi imeathirika. Kwa mfano vyombo vya habari ambavyo havipati mapato, utaona ajira zitapungua. Bila sekta binafsi hatuwezi kukuza uchumi,” amesema.
Akizungumzia ongezeko la kodi, mhariri Charles Misango ameitaka Serikali kuweka ukomo wa makusanyo ya tozo kama za simu na kuweka malengo ya matumizi yake.
“Baada ya vita ya Tanzania na Uganda, Mwalimu (Julius) Nyerere alitangaza miezi 18 ya kufunga mikanda. Hii pia tungweka muda, kwamba hii kodi lengo ni kukusanya shilingi ngapi. Hata barabara zitakazojengwa tujue zimejengwa vipi,” amesema.
Kuhusu punguzo la faini ya bodaboda kutoka Sh30,000 hadi 10,000, Misango amesema haina faida yoyote.
“Sioni mantiki ya kupunguza faini ya bodaboda. Ningeshauri iongezeke tena ifike hata Sh50,000 kwa sababu bodaboda ni kama wana nchi yao, wana utawala wao na hawana makosa. Ikitokea wamesababisha ajali wanaweza kuchoma hata gari lako. Kwa sababu wataona Sh10,000 ni kitu gani?” amehoji.
Awali wakichokoza mada katika mjadala huo, wataalamu wa uchumi wameipongeza bajeti hiyo na kukosoa katika baadhi ya maeneo.
“Kwanza niipongeze sana hii bajeti kwa sababu ni bajeti ya matumaini na inakwenda kumgusa kila mwananchi. Inatusogeza kufanya biashara kwenye uchumi wa kati,” amesema Lawrence Mlaki ambaye mchambuzi wa masualoa ya uchumi na fedha.
Naye mkufunzi wa udhibiti wa fedha binafsi, Edmund Munyagi amesema hatua ya Serikali kuongeza kodi na tozo itapunguza walipa kodi.
Chanzo: Mwananchi