Wahenga:Mnakumbuka Kishada/Tiara ?

Wahenga:Mnakumbuka Kishada/Tiara ?

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Nimekumbuka kitu kinaitwa kishada. Ni karatasi inakatwa na kutengenezwa mithili ya ndege kama Stealth Bomber za USA ila kishada kinakuwa na mkia mrefu.

Ukishatengeneza unakifunga na kama za ki-sulphate(kiroba) ndefu sana. Baada ya hapo mnakirusha kwa direction ya upepo. Tulikuwa tunaweza kurusha kishada kikaenda hadi km 5 away!

Starehe ingine ilikuwa kuteka kishada cha wengine. Mnatengeneza kamba ndefu mnaifunga jiwe mwishoni, halafu unarusha lile jiwe juu ya ksmba ya kishada mnachotaka kukiteka kazi kwesha!

Zama zile zilikuwa tamu sana!
 
457339618569a3beafaee20df8c02330.jpg

f4c1dc5c83da6d2c4f417ac11ac8ddf1.jpg

537f98bba5274f46adff6896deff00af.jpg
1102d29be2508eda19352b5b9e66fb54.jpg

e3172c6a97b00118cb5d384c322693b9.jpg

fb94f78b4a72f98be014f1820392f67f.jpg
 
Dah miaka hioo maisha yalipokua maisha!! Tulikua so creative, tulifurahia maisha like there is no tomorrow. Tulikamata panzi, tulitengeneza magari, tluifanya kila kitu kilichokuwa ndani ya uwezo weti ili tu kitupatie raha ya siku nzima. If I could turn back the time....
 
Kitambo, nakumbuka enzi hizo tulikuwa tunaenda kuokota mabunda ya uzi pale Tabata dampo na tulikuwa tukirusha kutoka Tabata Kimanga hadi Manzese kulingana na mwelekeo wa upepo alafu kwa juu unaandika ujumbe,ilikuwa 1987-1991 ndiyo burudani hii ilipotoweka kijijini kwetu Tabata.
 
Sisi tulikuwa tunatumia nyuzi za viroba, vi-sulphate
 
Dah miaka hioo maisha yalipokua maisha!! Tulikua so creative, tulifurahia maisha like there is no tomorrow. Tulikamata panzi, tulitengeneza magari, tluifanya kila kitu kilichokuwa ndani ya uwezo weti ili tu kitupatie raha ya siku nzima. If I could turn back the time....
Very creative...sasa hivi ule mchezo wa kupulliza bubble watoto wananunua mlimani city wakati sisi tulikuwa tunatumia vibomba vya majani ya mpapai na maji ya sabuni.
 
Wahenga pekee ndio tutaokuelewa ujue kuhusu kishada nakumbuka ni gazeti na kamba hiviiii nilikua
 
Back
Top Bottom