Nimerudi Mkuu!
Naomba nami niongezee katika kuweka sawa zaidi maswali yako kama wajumbe waliotangulia walivyoelezea ila ntajibu kwa kufuata mtiririko wa maswali yako japo swali namba 1 na 4yatajibiwa kwa pamoja.
1=>Maana ya 'grouo of companies' na makampuni mengine
Group of companies ni mkusanyiko wa makampuni zaidi ya moja ambayo yatakuwa chini ya kampuni mama ie holding company iliyotengenezwa kununua na kumiliki hisa za kampuni nyingine shiriki. Hii kampuni mama ikimiliki shea kubwa ndiyo huipa uwezo wa kuzidhibiti kampuni shiriki. Hii ina maana ya kwamba kampuni mama inakuwa na sifa hizi
a) uwezo wa moja kwa moja au si moja kwa moja kudhibiti, kuwa na nguvu ya kura ya maamuzi katika mkutano mkuu
b) kuwa na haki ya kuchagua kwa kuappoint au kudhibiti wakurugenzi ambao watakuwa na nguvu ya kimaamuzi katika mkutano wa bodi
c) kuwa na nguvu na haki ya kura ambazo zitaamua usalama na mustakabali wa kampuni shiriki
2=> Makampuni mengine yamegawanyika katika sehemu 3 ambazo ni kama ifuatavyo na maelezo yake kwa kifupi
a) kampuni binafsi
Ni kampuni yenye asili ya mahusiano ya kijamii zaidi kuliko ya kibiashara kabla ya kusajiliwa kwake. Mahusiano yanaweza kuwa baina ya ndugu katika familia n.k. Ni ngumu kusajiliwa katika masoko ya hisa na kuhamisha hisa ni ngumu vilevile. Ina kiwango cha umiliki kuanzia watu 2 na mwisho watu 50 tu
b) kampuni ya umma
Hii ni kampuni iliyowazi ambayo mtu yoyote anaweza anaweza kununua hisa na kuwa sehemu ya umiliki. Inaanzia watu 2 na haina mwisho. Inaweza kusajiliwa katika masoko ya hisa. Kampuni binafsi inaweza kusajiliwa katika masoko ya hisa iwapo marekebisho ya vipengele vta memorandum vitarekebishwa
c) kampuni ya kigeni
Ni kampuni iliyosajiliwa nje ya Tanzania lakini shughuli zake inafanyia Tanzania. Inaweza kuwa Tanzania kama tawi. Hata kama wamiliki wote Watanzania lakini imesajiliwa nje ya Tanzania itabaki kuwa kampuni ya Kigeni
2. Taratibu za kusajili kampuni
a) Jina la kipekee la kampuni lazima lisifanane na jina lolote linalo fanya biashara
b) Memorandum and Article od Association lazima zipokelewe na kukubalika BRELA
c) Kutimiza taratibu na sheria zote kwa mujibu wa fomu namba 14b na kiapo cha mwanasheria kithibitishe
d) Maelezo kamili ya wakurugenzi wa kampuni yawe yenye kujulikana kwa mujibu wa fomu 14b
Faida za group of companies ni
1. Kisheria
Uwezo wa kuthibiti kampuni shiriki kwa kupitia bodi ya wakurugenzi. Uwezo wa kuwaajiri na kuwafukuza kisheria menejana wakurugenzi wa kampuni mshirika
2. Uthibiti wa matumizi sahihi za rasilimali
3. Kupunguza uwezekano wa hasara / risks hasa kwa Multinational compnies
4. Mipango ya pamoja ya kodi katika kuangalia sehemu zenye kodi ndogo hivyo kufungua kampuni mshirika. Mfano kampuni A iwapo ikaona Tanzania kodi zimekuwa kubwa na nyingi sana inaweza kuhamishia sehem ya shughuli zake kwa kupitia kampuni B iliyopo Kenya ambako kuna unafuu wa kodi
5. Wakurugenzi na mameneja wa kampuni mshirika wanawajibika kwa kiwango cha juu sana kwani kampuni mama inauwezo wa kuwaondoa
Angalizo:
Nimejitahidi kutokutoa mifano ya majina ya makampuni kutokana na sheria na kuna baadhi ya wamiliki hawapendi kampuni zao kutolewa mifano
Nimejitahidi kutumia kiswahili ili kila mtu aweze kuelewa ili itusaidie kurekebishana
Maelezo yangu yame 'base' kutoka source ya Brela iwapo kuna mahala hapajakaa vema nirekebisheni kwani hakika ukamilifu ni wa Mwenyezi Mungu
Nawasilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app