IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
Wahenga hao walisema lini??
Na walimwambia nani??
Kwanza sidhani hata Kama hao wahenga walijijua kua wanaitwa wahenga!!!
Mi nadhani wahenga ni wazee waliotutangulia,ukiangalia wazee wa zamani kuna misemo yao mpaka leo tunatumia,haijulikani hao wazee ni kina nani ila wanaongelewa kwa ujumla.
umeniacha hoi mkuu.Wahenga ni wazee wa jiji la Dar es salaam!
Mi nadhani wahenga ni wazee waliotutangulia,ukiangalia wazee wa zamani kuna misemo yao mpaka leo tunatumia,haijulikani hao wazee ni kina nani ila wanaongelewa kwa ujumla.
Kila methali wahenga walisema.hivi hao wahenga walikuwa watu gani??
Wahenga ni watu wenye hekima, busara na uwezo wa kufanya mamuzi sahihi. Tatizo langu na mimi lipo hapo kwamba ni kama vile walikuwepo zamani tu na siku hizi hawapo. Wahenga walisema....kwa nini hatusemi wahenga wanasema?
Elders !! akina babu na akina bibi !Kuuliza sio ujinga,
Toka nimeanza kusama darasa la kwanza mpaka namaliza elimu ya juu sijui wahenga ni akina nani, mara utasikia mtu akisema wahenga walisema asiyesikia la mku…, wahenga walisema mwenda pole...
Wanajanvi naomba kujuzwa hivi wahenga ni akina nani?