Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

Sitaki kuikukumbuka ile dawa, sio kwa kuwashwa kule, siku tatu mtu unawashwa tu unajikuna tu kama mwendawazimu
 
Kutapika nyongo ilikuwa ni lazima, ile dawa jamani.....khaa!
 
umenikumbusha hapo kwenye kuwasha ila kuna dawa nilipewa calamine lotion ilikuwa inasaidia.
 
Hii dawa ndio ilinifanya nichukie dawa.
Nakumbuka nilikuaga nakunywa dawa bila kukunja sura mpaka siku nimerudi kutoka shule naumwa. Kufika bibi akanikorogea chai ya rangi akaniwekea na dawa (Chloroquine) nikanywa.. nilitapika isivyo kawaida. Kuanzia hapo nikachukia chai yenye sukari nyingi na sikuwahi kulamba tena sukari. Hata nikiona mtu analamba sukari nasisimkwa mwili. Nikaogopa dawa na kuchukia mpaka leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mamake hiyo dawa kuwasha kwake ni noma,nilishukuru nilipoanza kutumia fansidar ikawa inafanya kazi haraka bila kuwashwa na kutapika.
 

Kunywa Q-kwini bila Piriton ilikuwa haiwezekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…