IKUNGURU IJIRU CHUKU
JF-Expert Member
- Feb 27, 2021
- 484
- 545
1. Enzi hizo watu tulivaa viraka. Mafundi cherehani walipata kipato kwa kushona viraka. Suruali la baba lilikatwa kaptura za watoto na chupi kadhaa za mama.
2. Enzi hizo watu tulipiga mswaki kwa mkaa. Watu tulivaa kata mbuga. Miguu ilijaa funza wakubwa utadhani mbaazi. Tulikwenda chooni peku, tena wakati wa mvua na hatukuugua. Baada ya kujisaidia tulitumia gunzi la muhindi au kona ya ukuta. Hakuna maji chooni wala bafuni. Kujisaidia vichakani ilikuwa bora kuliko chooni. Tulimwagia majivu chooni kila siku asubuhi kupunguza harufu na kuua wadudu.
3. Enzi hizo watu walikuwa na chawa kichwani acha kabisa. Mayai yake yalizunguka kichwa kizima.
4. Enzi hizo tuliishi chumba kimoja na mifugo, bata, mbuzi, kuku, sungura, panya, nge na tulisavaivu. Tulitandika magunia na tulilala juu ya mavi ya kuku, mbuzi, kondoo, ila shukrani kwa mungu kwa ulizi wake wote mpaka leo hii.
5. Enzi hizo watu tulienda shule pekupeku, uku tukibeba , mifagio, madumu, vifuniko vya soda, njiti, huku kaptura ya shule ikiwa imechanika kwa nyuma imebakiza uzi wa katikati,hapo ndani hakuna chupi