Wahenga wenzangu tukumbushane adha tulizokuwa tunapitia kwa kutokuwepo simu za mikononi

Wahenga wenzangu tukumbushane adha tulizokuwa tunapitia kwa kutokuwepo simu za mikononi

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,415
Reaction score
119,473
Amani iwe kwenu. Aisee tumetoka mbali sana, ashughulikiwe aliyegundua simu hasa za mkononi.

Ilikuwa mtu unafunga safari kwenda kumtembelea mtu unakuta na yeye kasafiri.

Kupata taarifa za msiba ilikuwa shughuli kupata maana mtu anaandika barua inafika baada ya miezi mitatu. Nakumbuka sisi alifariki ndugu yetu mwezi wa nne taarifa tukapata mwezi wa saba.

Hata wachepukaji kipindi hiki walikuwa wanachepuka kwa ugumu sana tofauti na sasa.

My sister anasema mzee alikuwa anatembea kwa mguu hadi chuoni kwake kumpelekea pesa ya matumizi ( ni mwendo kama wa masaa nane)
Karibuni
 
Technology has improved and harmed the world. Hatusalimiani, hatutembeleani, yaani shida tupu, mkikaa watano kila mtu na smartphone yake, hatuandikiani barua tena, namiss zile zenys makopa.
 
Kama simu zingekuepo kama kipindi hichi ningekula tunda la Mwanne.

Aye hivi unajua ile unajubaliana na binti muonane kesho labda uwanjani saa saba? So unaenda pale saa saba halafu yanakata masaa hatokei and you ain't sure ikiwa uendelee kusubiri au usepe?

Zimenikuta mara nyiiiiiiiiiingi
 
Enzi hizo nakumbuka kuna mama mdogo wangu alikuwa anaishi kenya, alitutumia barua kututarafu kuwa anaumw, ilichukua mwezi mzima kuja kutufikia. Na apo inafika ameishakufa ana kama wiki mbili na tumeisha toka msibani. Yan bas 2 na enzi hizo ni sim za mezan tu na ilikuwa ni ghari kupiga sim nje ya nchi
 
Ilikuwa simple tu, ni kummendea kisimani afu unamwambia jua likizana tunakutaka chini ya mti wa muembe au wa mpingo au wa mninga basi inakuwa imeisha hiyo
Hapo kwenye uchepukaji nakazia.


Ilikua ngumu ngumu sana .

Saizi ni mitandao imerahisisha.
 
Back
Top Bottom