Wahindi wa TRL watoweka na mabilioni!

M-bongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
338
Reaction score
71
Taarifa nilizozipata punde toka chanzo cha ndani kabisa kwa maana ya mtumishi wa TRL makao makuu ni kuwa wale vibosile wa TRL ambao ni wahindi wametoweka na kiasi kubwa cha fedha na kubakiwa wahindi wachache wa kada za chini ambao hata hivyo nao wamekuwa wakiondoka mmoja baada ya mwingine, naomba kanzi kafanye kazi hii ili kuthibisha ukweli huu au yeyote mwenye access na TRL atujuze juu ya tetesi hizi
 
Sasa wafanye nini maana Tanzania Ni shamba la bibi...!! Tunaomba Habari zaidi bwana mzee
 
Inatia Hasira sana na mambo ya ajabu yanyoendelea Tanzania kwa sasa ndugu zangu kama ni kweli nini cha kufanya ndugu zangu
 
loh sitashangaa kabisa kama ni kweli kwani wangapi wamejichotea hawajatoroka na bado hakuna nayewachukulia hatua ni wale walioenda makwao.
 
Yes taarifa nilizozipata muda si mrefu ni kwamba wakurugenzi wa TRL yaani wale wahindi wapo kwa mkataba wa muda mfupi.Hivyo mtoa taarifa kaniambia kuwa hawa jama wa na Account ambay mkurugenzi wa fedha ndo mwenye dhamana ya kudraw and kuitunza lakini chanzo cha hela hizo ikiwa ni mapato ya TRL na zile zinazotolewa na serikali.

Hivyo Huyo mkugenzi wa fedha alipomaliza mkataba wake akajifanya anaeinda kuchukuwa vipuli huko kwao india ndo akdraw hela zote kwenye ile confidential account na kutimkia huko.

Hizo nd taarifa nilizozipata wakuu.
 
Singependa kuamini hii habari, na kama ni kweli basi itakuwa scandal kubwa sana:
"
RITES, a Government of India Enterprise, provides comprehensive engineering, consultancy and project management services in the transport infrastructure sector under single roof. Since its inception in 1974, company has made steady progress and diversified into new areas of business such as, export/leasing, maintenance and rehabilitation of railway rolling stock, operation and maintenance of railway systems under concession agreements and BOT, BOOT and PPP projects.

Presently, we have over 600 on-going projects in India besides over 30 projects overseas". www.rites.com
 
Kila issue ya wizi wa mamilion mhindi(Watanzani wenye asili ya Asia) hakosekani yaani hawa mpaka tuko.
Hivi yale mabomu ya Mbagala ntapata wapi nikajimalize pale upanga na kaliakoo naweza wapunguza.
 
Waliambiwa kuwa Kampuni hii ni Kisanii sana na wao wakasema kuwa ni uongo na maneno ya Mitaani sasa Tazameni nyinyi mwenyewe
 
hata kama ni shamba la bibi, serikali ianze kuwatia pingu Wabongo waliofanikisha mpango ule -- Sir Andy Chande (sijui kwa nini Mzee Mengi hakumtaja mdosi huyu katika ile list yake ya 'mapapa') na Andrew Chenge -- kama alipona kwa radar, basi hili asipone. Mwingine ni BWM.

Serikali yetu na angalau iamke kidogo na kujali jinsi wananchi masikini wanavyoibiwa na ianze kamata kamata.
 
Kila issue ya wizi wa mamilion mhindi(Watanzani wenye asili ya Asia) hakosekani yaani hawa mpaka tuko.
Hivi yale mabomu ya Mbagala ntapata wapi nikajimalize pale upanga na kaliakoo naweza wapunguza.


Taratibu Buswelu!! yani nimecheka mpaka basi. Hii ndio Tanzania zaidi ya tuijuavyo. Kama hii issue ni ya kweli sitashangaa na punde tume itaundwa na wala majibu sidhani kama yatapatikana.
 

Hawa Rites ndio waliokuwa na mkataba na Tanzania?..mbona hata kwenye website yao hakuna project yeote na Tanzania,bli nchi nyingine?...kama ifutavyo
RECENT CONTRACTS SECURED
--------------------------------------------------------------------------------
HOME:

Design consultancy for Quazikund-Baramulla railway project - IRCON International Limited

Project Management consultancy for Grade Separated Interchanges at 4 junctions at Sector XIV intersection at NOIDA - NOIDA Authority

Development of Industrial Estate at Bawal (Rewari) Phase-II - HSIDC

Detailed geotech investigation for design & construction of major bridges between KM 30 - 120 on Katra-Quazikund section - Konkan Rail Corporation Ltd.

Detailed engineering and construction management services for construction of additional railway infrastructure required for proposed track hopper for upcoming 5 & 6 unit (2X250 MW) of Mejia Thermal Power Station - Damodar Valley Corporation

ROB at Narender Nagar - Maharashtra State Road Development Corporation

Construction of railway infrastructure facility for 2X250 MW Thermal Power Plant at Korba (East)

Turnkey consultancy and construction supervision of the proposed railway siding at Dharwad - RJ Agro

Project Management consultancy on Deposit Basis, New Delhi - National Small Scale Industries Corporation Ltd.

Project management services for infrastructure facilities at IAF Station - Sirsa, Halwara, Hasimara, Kalaikunda, Bidar, Bareilly, Bhuj, Jamnagar and Hyderabad - M/S. Bharat Electronics Ltd.

Consultancy services for design of station building, quarters, ancillary structure and preparation of Master Plan Quazikund-Baramulla New Kashmir Line Project - IRCON International

Project Management Consultancy services for construction of ROB and New Link Road at Dadri (UP) - Greater NOIDA Authority

NIMECHANGANYIKIWA, NAOMBENI MSAADA
 

Yametimia, na hili tulilitegemea tu!. Kwani watu walisema weeeeeee, lakini tukaishia kuambiwa RITES ndo mkombozi, kumbe Mkombaji!
 

Wajinga ndio waliwao
 
Taratibu Buswelu!! yani nimecheka mpaka basi. Hii ndio Tanzania zaidi ya tuijuavyo. Kama hii issue ni ya kweli sitashangaa na punde tume itaundwa na wala majibu sidhani kama yatapatikana.

Tume itakuwa ya kuficha majibu na kuondoa ushaidi na sio kuwaambia wananchi au bunge butu nini kilichotokea.

ONLY in Tanzania! My Beloved Country!
 
Taratibu Buswelu!! yani nimecheka mpaka basi. Hii ndio Tanzania zaidi ya tuijuavyo. Kama hii issue ni ya kweli sitashangaa na punde tume itaundwa na wala majibu sidhani kama yatapatikana.


Tshala kama ulikuwemo tena usikute ukawa mjumbe wa hiyo tume uchwara. Hivi ile nyingine ya mabomu ya Mbagala ilshatoa report? Hili linawezakana bongo peke yaani Jeshi limechemsha lenyewe ndio linatuhumiwa lakini jeshi hilo hilo ndio linafanya uchunguzi ili kutoa hukumu kwa jeshi-huu kama si uchizi ni nini tena? Hivi Nyerere tulimkosea nini jamani maana nahisi kama ametuachia laana vile?
 
Kweli wajinga ndio waliwao kila mtu anajijia tu kuchota na kuondoka zake hawa wahindi vipi, ina maana hakukuwa na kiongozi yeyote MTZ kwenye ngazi ya juu kweli inaudhi kwamba wanaachia mambo yanaenda mlama-Ehe Mungu wetu tusaidie tumekwisha Tanzania
 
duh! Kweli serikali ya Tanzania ni hovyo. Nchi inaliwa kila siku, na kelele zinapigwa bure. Tunakuwa kama tunapigia mbuzi gitaa. Jana nilikuwa nasoma habari ya hawa na kukodisha injini zao zitumike na TRL kwa laki sita kwa siku/mwezi. Nimechoka kabisa!! Basic, basic things vinatushinda. Ivi wanasheria wa serikali wanafanya kazi gani?
 
kila siku kuna scandal mpya ,hii nchi tukifanya masiala itakuja kufirisika kila kitu kwa speed hii.
 
Tunajaribu kutafuta ukweli wa issue hii, kama itabainika ni kweli ama si kweli hatutasita kuwafahamisha...
 

Juu ya Mkapa mbona bado mnamuandama? Si aliwaabia kuwa "MITANZANIA mingine ina wivu wa KIJINGA?". Sasa hadi leo bado mnamuonea wivu wa KIJINGA tu huyu mzee? Pia Muungwana kawaambia mwacheni Mzee Apumzike na zile 20% alizopata kwa kuuza mali za Watz.

Mnaona wivu watoto wake wanavyofaidi ehh? Mnaona wivu Wahindi wanavyoteka mahela na kulala nayo mbele ehh? Mnaona wivu watu wanavyoishi maisha tambarale siyo? Jinsi Barrick Gold inavyokula maisha hapa ehh?

Acheni WIVU WA KIJINGA, WATANZANIA NYIE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…