Wahindi wa TRL watoweka na mabilioni!

kweli hili ni balaa, lakini inakuwaje wananchi wa kawaida tutaona kabisa hiki kitu hakifai lakini serikali na viongozi wakuu wanakuwa ndio mstari wa mbele kuwatetea, hivi kwelim kuna mwekezaji gani kweli anawekeza lakini hana hata pesa anatregemea asset ulizompa aende kukopea pesa,
 
Hili si Swala la mchezo. Inabidi Serikali iwe taugh sana.

- Kuna Terms na Conditions Zilisainiwa

- Katika mikataba kama hii, je Serikali RITES waliweka Performance Security? Kama ndiyo basi tudai fidia.

- Je kwa kutoroka kwao wamevunja au ku-breach mkataba, kama ndiyo basi inatakiwa washtakiwe.

- Kama ni kweli pesa za TRL ziliweka katika kampuni tofauti na mkataba unavyosema basi wawajibishwe kisheria.

- Kama kulikuwa na mizengwe, basi uchunguzi ufanyike na wote waliohusika na uzandiki huu, wachukuliwe hatua za kisheria.

Hivi Sir Chande atakuwa mbali na Mkenge huu kweli?
 
Waliambiwa kuwa Kampuni hii ni Kisanii sana na wao wakasema kuwa ni uongo na maneno ya Mitaani sasa Tazameni nyinyi mwenyewe

Unadhani walikuwa hawajui kwamba hawa RITES ni wasanii? Wajanja wameshagawana 10% za hiyo pesa hapo, nyie mtabaki kudhani kuwa serikali ilikuwa haijui. Rushwa ni mbaya sana kuliko tunavyoweza kufikiria. Inanunua utu wa mtu kabisa!
 
duh! letu jicho tu.. spika nae hahusiki?,maana naskia anafukuza wanaosema kweli bungeni..
 
unajua nchi yangu tanzania haina dira, viongozi sijui wakoje
hawa si ndo serikali ilikuwa inawasaidia kulipa mishahara????!!!!
sasa yako wapi?
 
unajua nchi yangu tanzania haina dira, viongozi sijui wakoje
hawa si ndo serikali ilikuwa inawasaidia kulipa mishahara????!!!!
sasa yako wapi?

RUSHWA RUSHWA RUSHWA...........Inawafunga midono viongozi wetu! Hakuna kingine! Hapo ilitembea rushwa tu!
 

Maskandali makubwa mangapi yameishatokea hapa nchini kwetu na yamebaki hadithi tu? Na hili litapita.
 
Kwani sisi hatukuweza kuendesha shirika la reli mpaka waje wahindi? Wasomi wetu wamekwenda wapi? Vyuo vikuu vinafanya nini...havitoi graduates?
 
Sijaelewa hizi mamlaka zinahusika kama kweli zipo au wanajua uchaguzi mwakani??
 
tatizo viongozi wetu ndio wamekuwa sehemu kubwa ya kuchangia matatizo kuliko kutatua matatizo.hawana mapenzi na nchi yetu.
 
Dingswayo:
Kwani sisi hatukuweza kuendesha shirika la reli mpaka waje wahindi? Wasomi wetu wamekwenda wapi? Vyuo vikuu vinafanya nini...havitoi graduates?

Havitoi graduates -- vinatoa makada wa CCM ambao ni mafisadi watarajiwa.
 
Kipindi cha kuelekea uchaguzi ndio kipindi cha kuchuma shambani kwa bibi........
 
Kila issue ya wizi wa mamilion mhindi(Watanzani wenye asili ya Asia) hakosekani yaani hawa mpaka tuko.
Hivi yale mabomu ya Mbagala ntapata wapi nikajimalize pale upanga na kaliakoo naweza wapunguza.

wewe ni ubaguzi
jieleze kwa nini tusikufungie JF

Buswelu umechemsha
 
Last edited:


Serikali inashindwa kuwatia nguvuni watu wa EPA , Deep green, Meremeta nk itawezaje kwa wahindi ?
 

Kumbuka Chande nikiongozi wa Free masons wa Tanzania.kama unajua kinachoendelea Tanzania google neno free masons ukishajua hao wana nguvu gani na ni watu wa hatari kwa jinsi gani ndo utajua kinachoendelea Tanzania hivi sasa.

baadhi ya watu mashuhuri na mafisadi kama wanavyoitwa na watanzania wamejiingiza katika kikundi hicho cha hatari sana.

kikundi hicho cha Free Masons kilichoanza miaka ya 1800 huko Ireland kinajumiusha maraisi wafanya biashara watu mashuhuri na shughuli zake ni za siri ukugundulika unafuatilia mtandao wao utapotea.... miongoni mwa wanachama maarufu ni kina George Washington rais wakwanza wa Marekani.

Basi naishia hapa ili nikupe nafasi ya kuchimba habari za watu hawa hatari kwa dunia nzima pamoja na kikundi kingine cha Illuminant.
 
Yametimia, na hili tulilitegemea tu!. Kwani watu walisema weeeeeee, lakini tukaishia kuambiwa RITES ndo mkombozi, kumbe Mkombaji!

Waliokomba Richmonduli mbona bado wako bungeni,kina vijisenti pamoja na kashfa nzito bado wanakomba kodi ya mlalahoi bungeni.waliokomba kiwira leo hii wanapigiwa debe badala ya kuachwa wajitetee kwa watanzania.
Hiyo ndo nhi ya wadanganyika."Shamba la Bibi".Inahudhunisha mno,
hakuna jinsi wananchi watainusuru nchi hii kama wasomi na wanaharakati hawatajikita vijijini na kuenda kuwafungua upofu waliogubikwa kwani mchango mkubwa wa viongozi wabovu hutokea huko vijijini ambapo bado wanafanya uchaguzi kwa ushabiki kama vile kuna timu mbili uwanjani.
 
Hivi hii serikali yetu imelala usingizi kiasi hiki kweli wanaosema Tanzania ni shamba la bibi hawajakosea. Waunde tume ya nini cha kwanza ni kuwaweka ndani wote waliohusika na mkataba huu watajieleza mbele ya safari wasitufanye sisi wajinga. Kikwete anayaona haya lakini yeye kutwa nzima ni safari tuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…