Wahindi wameua Mpira wetu Tanzania.

Wahindi wameua Mpira wetu Tanzania.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Klabu kubwa za Simba na Yanga ndizo ambazo zingekuwa chemchem ya soka letu Tanzania, bahati mbaya wanachama na wapenzi wa timu hizi waliwaachia wafanyabiashara wa kihindi kufanya biashara na kufaidika na timu hizi kwa mgongo wa ufadhili.

Wafanyabiashara hawa walijali faida badala ya maendeleo ya soka. Walicheza kamali na matokeo ya mechi za Simba na Yanga hivyo walifanya kila kitu na kila mbinu ili kulazimisha matokeo uwanjani kitu kilichodumu hata leo.

Wanachama na mashabiki hawalipi hata michango yao wakitegemea mhindi kuendesha club yao. Akina mzee Akilimali na wenzake hadi leo huwaambii kitu kuhusu timu kujitegemea, wanatafuta mfadhiri wa kihindi aje awape furaha ya uwanjani hata ikibidi kwa kununua mechi.

Hivyo Mpira wetu ulibaki chini kwa tabia hii mbovu ya kupenda matokeo ya leoleo ya uwanjani kutoka kwa wahindi.
 
Wa kujilaumu ni sisi wenyewe wala sio wahindi kuna wasomi na watalaam wengi tu wenye mawazo ila hawapewi nafasi badla yake vilabu vimegeuka uwanja wa rushwa na biashara haram
 
Wa kujilaumu ni sisi wenyewe wala sio wahindi kuna wasomi na watalaam wengi tu wenye mawazo ila hawapewi nafasi badla yake vilabu vimegeuka uwanja wa rushwa na biashara haram
Kwa kutumia simba na yanga kuna watu walikwepa kodi, kutoa rushwa na kuuza na kutumia madawa ya kulevyà
 
Kwa kutumia simba na yanga kuna watu walikwepa kodi, kutoa rushwa na kuuza na kutumia madawa ya kulevyà
Na mpaka leo wanafanya hivyo na ndio maana ukienda pale na ushauri wa kitaalam watu wanaangalia kwanza kama unawafaa au la wakiona unaziba mianya ya wao kupiga pesa watakufanyia kila fujo ikiwemo kuharibu mechi ili ufukuzwe kwani si huyo Lwandamina kasema kifupi ni upuuuuuzi mi ni yanga ila amini usiamini tufungwea au tusifungwe sishtuki maana tukishinda sijui ni kwa nini na tukifungwa sijui ni kwa nini?
 
Simba na Yanga zina miaka 80+ lakini hazina vitaru vya kukuzia vipaji wala viwanja kwa kuwa hivyo sio vipaumbele kwenye biashara ya uwekezaji wa mfadhili. Mfadhili anataka matokeo ya leoleo kwa kununua wachezaji, makocha, marefaree, wajumbe wa TFF.
 
Simba sasa hivi wameweka kisambusa kwenye lift ya Mo hawana shaka kama ilivyokuwa kwa wenzao Yanga kwa Manji. Manara na wenzake wanachonga na kufurahi hataree mhindi anafanya mambo, hata kadi zao wanasubiri kulipiwa wakati wa uchanguzi wa mwenyekiti mpya.
 
Haya mhindi Manji amejiweka pembeni, kinachowazuia Yanga kupata maendeleo ni nini? Wakija kusaidia tatizo wakikaa pembeni tatizo. Mnataka wafanyeje?
Arudi tu jamaa hawana plan B ya kuiendesha tima mbali na kukinga mikono kwa wahindi.
 
Huu ndo wakati ambao mtani (jirani) kabanwa hana pa kuhemea! Ukija uwanjani hawana uhakika wa kuchukua kombe lolote. Ukienda kwenye makazi yao hawana hata pa kulala maji yamejaa hadi kwenywe dari. Ni shiida pole sana majirani
 
...Hivyo Mpira wetu ulibaki chini kwa tabia hii mbovu ya kupenda matokeo ya leo leo ya uwanjani kutoka kwa wahindi.
Tangu lini klabu ikakua bila kuwekeza fedha? Kama Mhindi anatoa ufadhili na pia kujinufaisha, na timu inapata matokeo ya hapo hapo, tatizo liko wapi? Nani anaweza kusimama na kupuuza mchango wa Azim Dewji kwa mafanikio ya Simba kuingia fainali ya CAF mwaka 1993? Nani anaweza kupuuza mchango wa YM kwa Yanga na kuiwezesha kucheza hatua ya makundi klabu bingwa Africa? Tuache wivu, wahindi wanajua biashara, jambo la msingi ni weusi kutengeneza mfumo utakaowawezesha kufanya biashara ya uwekezaji, kama ambavyo Simba imefanya sasa hivi
 
Huu ndo wakati ambao mtani (jirani) kabanwa hana pa kuhemea! Ukija uwanjani hawana uhakika wa kuchukua kombe lolote. Ukienda kwenye makazi yao hawana hata pa kulala maji yamejaa hadi kwenywe dari. Ni shiida pole sana majirani
Mkuu mbona hata simba ni hayohayo tu imekaa miaka kadhaa bila ubingwa tatizo ni utegemezi na hats sasa HV akiondoka Mo hali inabaki km yanga tu.
Kumbuka hata Mo bado issue ya kuichukua timu ni tata sababu ya sheria ya serikali ya 51% kwa 49%.
 
Back
Top Bottom