Wahisani wanasubiri hukumu ya Mbowe na wao watoe hukumu yao kimyakimya au vinginevyo

Hongera kwa kutetea, kwa nguvu zako zote, viongozi wa chama cha siasa chenye itikadi na malengo ya kitaifa, lakini wao wakikitumia kwa maslahi binafsi.

Kimsingi, Wanachama na Wafuasi wa hao viongozi, wamegeuzwa misukule. Hawahoji kauli na matendo machafu ya hao viongozi wala kukemea. Kutwa ni kuwapamba kama vile wao ni malaika.

Kwa bandiko lako hilo unaomba hao wadau wa maendeleo wasitishe ili iweje? Napende nisiamini kuwa hata wewe, hapo ulipo, unaishi maisha tegemezi na unayafurahia. AIBU
 
Hilo mbona lipo wazi ila viongozi wanatoa matamko wakidhani kuwa wahisani wataongea chochote kumbe wanataka kuungana kujitoa kuisaidia Nchi yetu kitendo cha Denmark rafiki wa kweli Tanzania na miradi ya maji toka enzi za miaka ya 80 ameamua kutoka kwa sababu ya ujinga wetu nimeumia sana...
 

Mwezi wako umeandama,umeanza kuwainamia wazungu wako. Mtoto wewe siyo riziki kabisa . Wafuate huko hao wazungu wako unaowaabudu wakakufanye wanayokufanya.
Sisi hapa kazi inaendelea
 
Ni kweli wamehudhuria kufuatilia kesi inavyoendeshwa, akipatikana na hatia, nao wataikubali hukumu iwapo ushahidi utakuwa na nguvu, lakini kama hakuna ushahidi ni yale yakubambikizana basi tusikia kelele zao, na hata sie tusio chadema tutapaza sauti.
Mkirindi naona akili zimekurudia nowadays, naungana na wewe! Kinachofanyika ni kulichafua Taifa na sio kuikomoa Chadema. CCM wana akili za ajabu sana
 
CCM ndie baba wa slave mentality, kila siku bakuli ulaya karibia miaka 60 baada ya uhuru.
Hiyo ni win win situation bro. Siyo nyinyi mnaotegemea mabeberu watawaingiza Ikulu ndiyo maana kuna viongozi wenu wanalelewa huko Ubelgiji.
 
Ni kweli wamehudhuria kufuatilia kesi inavyoendeshwa, akipatikana na hatia, nao wataikubali hukumu iwapo ushahidi utakuwa na nguvu, lakini kama hakuna ushahidi ni yale yakubambikizana basi tusikia kelele zao, na hata sie tusio chadema tutapaza sauti.
we ushaona wapi ufadhili wa ugaidi wa laki sita?
 
Kama hujui kaa kimya sasa.. hakuna ufadhili wa ugaidi wa laki sita?
Inaelekea hujui kabisa concept ya ugaidi na matendo ya ugaidi.

Hivi unahitaji shilingi ngapi kununua madumu ya petroli ya kuteketeza jengo, filling stations? Laki 6 haitoshi kufanikisha hilo?

Hujawai kusikia magaidi wanalipua vyombo vya usafiri wa umma kwa kutumia mabomu yaliyotengenezwa kienyeji na yanaleta maafa makubwa?. Jifunze zaidi concept ya ugaidi ndugu
 
Kwa sitahili hii tujiandae tozo kuongozeka make misaada imeshaanza kukata na mikopo ya riba nafuu hakunu kila mwenye uelewa anaona tunakoelekea mdogomdogo tu tutaelewana
 
CCM ndie baba wa slave mentality, kila siku bakuli ulaya karibia miaka 60 baada ya uhuru.
Waafrika tuna nguvu na tunatumia nguvu kuliko akili. Mwenye akili anaweza kumdhibiti mwenye nguvu hadi amfunge kamba asipate pa kupenyea.
Sasa, ni vizuri tuone umuhimu wa kutumia akili ili kumshinda atumiaye maguvu.
Tulipelekwa utumwani si kwa sanabu waliotukamata walikuwa na nguvu, la hasha, walikuwa na akili
zaidi yetu.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…