S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Kuna midaharo mbali mbali inayoendelea, mojawapo ni hili la WAHITIMU wengi wa vyuo VIKUU kuwa hawaajiriki kutokana na elimu mbovu wanayoipata vyuoni, kwa hiyo inakuwa ni vigumu kupata ajira.
Sawa,nakubaliana na sababu hii; lakini lazima tujiulize maswali mengi sana katika enzi hizi. Kuna idadi kubwa sana ya WAHITIMU ambayo haiendani na Taasisi tulizo nazo hususani hapa Tanzania kwenye sekta karibu zote.
TCU ndiyo wanaoshangaa na wanasema WAHITIMU wanasoma mitaala ambayo haiendani na uhalisia au mazingira. Swali ni kwamba hawa ndio wanabariki mitaala yote ya vyuo VIKUU baada ya kuandaliwa na chuo husika.
Changamoto iliyopo vyuoni ni masomo yanayofundishwa vyuoni, binafsi naona ni mazuri, kinachohitajika ni kusisitiza kwenye uhalisia na si kujikita kwenye nadharia tu.
Lazima magwiji wa kada mbalimbali Tanzania Ma Dr. Na Ma Prof. wajikite katika tafiti na wanafunzi wasome kutokana na tafiti za kisasa na si kung'ang'ania kusoma vitabu vya akina Plato, Socrate, Karl Marx na wengine bila kupambanisha bongo zao/zetu kuendana na uhalisia uliopo.
Pili, kukosa Taasisi zenye kuwapokea hawa WAHITIMU kwa sasa tofauti na zamani hii ni changamoto katika upatikanaji wa ajira.
Lazima sasa tuanze kuandaa mitaala itakayowafanya wanafunzi WAHITIMU wa vyuo waweze kujiajiri wenyewe.
Serikali iandae mazingira rafiki kwa hawa WAHITIMU kuanzia vijijini na mijini. Na si kujidanganya eti wawekezaji wataandaa hayo mazingira.
Serikali lazima ijue kuwa bila tafiti za maana vyuoni hakuna maendeleo na tukipuuza tafiti hatutafika tuendako kama Taifa. Kinachofanyika sasa ni kutegemea tafiti za mataifa ya nje na hii ni hatari sana kwa mustakabali wa elimu yetu.
Lazima wanafunzi wa vyuo VIKUU wajiamini. Pia, wahadhiri nao lazima wajikite katika kutoa elimu iliyo bora na si kusaka pesa tu. Ukiona chuo hakifanyi tafiti kama chenyewe ni hatari sana.
Ukiona Ma Dr. Na Ma Prof. vyuoni hawafanyi tafiti bila dili la maana toka nje ya nchi hasa nchi zilizoendelea ni hatari zaidi.
Tafakari sana.