kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kuna vijana wahitimu wa vyuo vikuu wengi wameajiriwa kwa mikataba ya kujitolea serikali za mitaa serikali kuu na mashirika ya umma.
Hakika inauma sana unapoona mtu amesota miaka miwili halafu nafasi imetoka anaomba halafu anapewa mtu mpya hajatoa jasho lolote kujitolea.
Kwa vyovyote yafaa mwenye kujitole na uzoefu wake kupewa uzito wa alama kwenye usaili au aliyejitolea uwepo utaratibu wa tofauti ili nafasi zikitoka aweze kuajiriwa.
Vinginevyo kwa hakika serikali kama watu binafsi haiwezi kuepa lawama ya kuonekana inashiriki kunyonya nguvu kazi ya vijana wahitimu na kufanya upendeleo wakati zikitokea nafasi za ajira.