A
Anonymous
Guest
Habari yenu Jamii Forums, naona wadau wengi wamekuwa wakisaidika kupitia jukwaa hili, naomba unipazie sauti
Mimi ni muhitimu wa Diploma (ambaye nasubiria kufanya Graduation mwezi December 2024) kutoka Institute Of Adult Education iliyopo Barabara ya Bibititi Mohammed, Posta Dar es Salaam, ni Taasisi inayotoa Elimu kwa Walimu wanaojiendeleza japokuwa wanazidi kuongeza course mbalimbali ambazo si tu kwa Walimu peke yao..
Changamoto yangu (yetu) ni kwamba kuna ukakasi wa Wanachuo kusajiliwa kwenye mfumo wa NACTVET baada ya kujiunga na chuo hicho ili pale tunapohitimu tupewe AVN kwa ajili ya kujiunga na vyuo vingine au kuzitumia kwenye kuombea mkopo wa Elimu ya juu.
Kwasasa Tunapojaribu kuomba kuomba AVN kupitia mfumo wa NACTVET, mfumo unatupa majibu ya "INFORMATION MISSING" kwa maana ya kwamba hatutambuliki, na badala yake huwa wanasajili wachache sana kwenye huo mfumo na baadaye sisi ambao hatujasajiliwa tunaambiwa tusubiri tutasajiliwa taratibu hali ya kuwa watu wana mipango ya kujiendeleza kwenye Vyuo mbalimbali.
Wanatulazimisha kubaki palepale wakidai tusome Degree mpaka tukimaliza na hayo matatizo ya kutofahamika kwenye mfumo wa NACTVET yatakuwa yameisha, (hii shida sisi sio wa kwanza kukumbana nayo, wengine waliomaliza miaka ya nyuma wameamua kukaa kimya sababu tayari wapo makazini yani ni walimu walioajiriwa tayari il kwa sisi vijana mpaka tunajuta kusoma pale😢).
Huwa ni wakali sana tusipo lipa Ada kwa wakati mpaka kufikia kuzuiliwa kuingia Darasani kusoma, lakini kumbe hata wao majukumu yao hawayakamilishi kwa wakati, kama hapa, mimi binafsi nimeshindwa kuendelea Degree kwa sababu hiyo hapo juu na hatujui hatma yetu sababu wanapasiana mipira tu.
Tulishafika mpaka Mwenge kwenye Ofisi za NACTVET wao wanadai hawama shida ila Taasisi yetu ndio inachangamoto, ila ukiwasikiliza Taasisi nao wanasema shida ipo huko NACTVET.